Waandishi wa habari wametakiwa kujipenda,kujiheshimu na kujitambua sanjari na uzalendo wa kuandika mema yanaofanywa na serikali yao kwa kuandika habari chanya zitakazosaidia mabadiliko katika jamii.
Akizungumza Mkurugenzi wa Menejimeti na Maarifa wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt.Philbert Luhunga kwa waandishi wa Habari na Watafiti, wakati wa mafunzo yaliondaliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) amesema kwamba ipo haja kubwa kwa wanahabari kupenda nchi yao kwa kutangaza mazuri yayoendelea kufanywa na serikali.
Alisema kwamba Taarifa mbaya utakazozitoa hazijengi nchi yako kwenye jamii hivyo tuangalie vizuri sana weledi uzalendo na kuipenda nchi yetu na serikali yetu kwa kutokosoa kosoa tu kwa kujikita kuandika mema yanayotendwa na serikali kuwaletea wananchi maendelea na kukuza vipato vyao.
"Mwandishi mwenye uzalendo kwa nchi yake ni yule anayejitambua kujipenda na kujiheshimu na kuandika habari chanya kwa maslahi mapana ya nchi yake,hujawahi kusikia mwandishi wa habari wa Marekani hukuti akikosoa kosoa nchi yake wanatanguliza maslahi ya taifa lao mbele,tujikite zaidi kuandika habari Positive"
kwa mujibu wa Dkt.Luhunga ametoa wito kwa waandishi wa habari lazima wajue kwamba hawana nchi nyingine isipokuwa Tanzania hivyo ni vyema wakaandika mema ya nchi yao kuandika habari njema zinazofanywa na serikali yao ni Jambo jema.
Awali Afisa uhusiano na mawasiliano Tume ya taifa ya Sayansi na Teknolojia Faisal Abdul amesema kwamba ziara ya mafunzo kwa watafiti kuandika habari za Utafiti utasaidia kujua mafanikio ya Sayansi na teknolojia yanaotekelezwa hapa nchini kupitia taasisi hiyo.
Ameeleza kuwa taasisi hiyo imejikita kuwasaidia wadau wa maendeleo wakiwemo watafiti na wabunifu waliojikita katika sayansi na teknolojia ikiwemo kuwawezesha fedha kwa makundi hayo ili kuleta mabadiliko chanya.
"COSTECH imejikita zaidi katika kuhakikisha inawezesha tafiti nchini zinaleta majawabu chanya katika sayansi na Teknolojia sanjari na Ubunifu ndio maana tumewashirikisha watafiti nanyi wanahabari ili kuweza kutangaza tafiti hizo mkiwa na mafunzo yatasaidia Sana kuboresha na kuwafikia walengwa "amesema Faisal
Mafunzo hayo yaliowashirikisha wanahabari na watafiti zaidi ya 40 wa mikoa ya kanda ya kaskazini kuripoti habari za kiutafiti
Post A Comment: