Na Ahmed Mahmoud,Arusha
UFINYU wa chumba cha kuhifadhia Watoto Njiti katika Kituo cha Afya Levolisi unasababisha baadhi yao kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mount Meru
Akizungumza jana wakati wa upokeaji wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na wanawake kutoka taasisi na mashirika mbalimbali ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku wa wanawake Duniani yenye kauli mbiu ya “Kizazi cha Haki na Usawa kwa Mandeleo Endelevu , Tujitokeze Kuhesabiwa “
Dk, Anthony Mmao ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa chumba hicho hali inayopelekea Watoto wengine kukimbiwa hospitali ya rufaa Mount Meru kwaajili ya uangalizi maalum
“Kituo hiki kinahifadhi watoto njiti 7 hadi 10 jambo ambalo idadi ikizidi inasababisha Watoto hao kikimbizwa hospitali ya mkoa hivyo endapo upanuzi wa chumba hiki ukifanyika tutawasaidia katika ukuaji wao”
Aliomba wadau mbalimbali kuwasaidia ili waweze kupata chumba kikubwa kwani kituo hicho kwa mwezi kinazalisha watoto 400 kwa mwezi jambo ambalo ikitokea dharura ya kuzaliwa mtoto njiti inabidi kukimbizwa katika huspitali hiyo ya rufaa
Alisema kituo hicho kinabiliwa na changamoto ya uzio kuzunguuka eneo hilo hali inayosababisha uchafu kutoka nje kuingia ndani ya hospitali
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Arusha, Yasmine Bachu akikabidhi vifaa hivyo kwaniaba wa mashirika na taasisi mbalimbali mkoani hapa alishukuru kinamama hao kujitoa kwaaajili ya kusaidia jamii yenye uhitaji na kusisitiza kuwa changamoto ya ufinyu wa chumba cha kuhifadhia Watoto hao ameichukua na kuifanyia kazi huku changamoto ya uzio aliahidi kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo kwaajili ya kuitatua
Alitoa rai kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki maadhimisho hayo ikiwa ni mwaka wa kwanza wa Rais Samia Suluhu akiwa madarakani hivyo wanawake wanajivunia kwa kumuunga mkono katika shughuli mbalimbali za kijamii na kimaendeleo
Awali, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Zawadi Ngairo alisema taasisi hiyo imetoa baadhi ya vitu mbalimbali kama mchango wao kurudisha fadhila kwa jamii huku Ofisa wa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha, Blandina Nkini alishukuru kwa misaada hiyo kituoni hapo na kutoa rai kwa wanawake hao kujitokeza kwa wingi kwenda kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwaajili ya kutangaza vivutio vya utalii
Pia alisisistiza kujitokeza katika matukio mbalimbali ikiwmeo usiku wa mwanamke, kongamano la siku ya wanawake na mbio za Fun Run za kilomita 5 na kumi zitakazoanzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hadi Uwanja wa Shekhe Amri Abeid
Mwisho
Home
Unlabelled
UFINYU WA CHUMBA CHA KUHIFADHIA WATOTO NJITI KITUO CHA LEVOLOSI INAPELEKEA WATOTO WAKIZIDI KUKIMBIZWA MOUNT MERU
Post A Comment: