Afisa Masoko (TBS) Bw. Mussa Luhombero akitoa elimu kuhusu majukumu ya TBS, umuhimu wa kusoma maelezo yapatikanayo kwenye kifungashio, umuhimu wa kuangalia mwisho wa muda wa matumizi katika bidhaa na namna ya kutambua alama ya ubora ya TBS kwa bidhaa zilizothibitisha kwa wanafunzi wa shule za Sekondari za Inyonga na Ilela wakati wa kampeni ya uelimishaji umma wilayani Mlele-Katavi Afisa Udhibiti Ubora (TBS), Bw. Emmanuel Mushi akitoa elimu ya jinsi ya kutambua bidhaa zilizothibitishwa na TBS,umuhimu wa kusajili majengo ya chakula na vipodozi, pamoja na kuzingatia muda wa mwisho wa matumizi ya bidhaa husika kwa wananchi na wafanyabiara wa soko la Mlele wilayani Mlele-Katavi wakati wa kampeni ya elimu kwa umma.

*************************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) laendelea na kampeni ya uelimishaji umma kuhusu masula ya viwango katika ngazi za wilaya ambapo limwezeza kutoa elimu hiyo katika wilaya ya Mlele kwa wanafunzi wa shule za msingi, Sekondari na wananchi katika masoko na Stendi.

Akizungumza wakati wa kampeni hiyo Afisa Masoko TBS Bw. Mussa Luhombero amesema, Shirika lilianzisha kampeni hii mwaka 2017 lengo likiwa nikuwafikia wananchi mahala walipo na kuwapa elimu hii ambayo inafaida sana katika maisha ya kila siku ya mtanzaia kama mlaji wa mwisho kwa bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zitokazo nje ya nchi

" Elimu hii itolewayo na TBS inafaida kubwa kwa wananchi kwani inaongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa viwango kwa bidhaa zizalishwazo, umuhimu wa kuangalia muda wa mwisho wa matumizi ya bidhaa, na umuhimu wa kuhifadhi chakula na bidhaa za chakula katika majengo yaliyosajiliwa na TBS"

Endapo elimu hii itazingatiwa vyema na wananchi suala za uuzaji wa bidhaa hafifu, na zilie zilizokwisha muda wa matumizi sokoni litapungua kama sio kuisha kabisa. Alisisitiza Bw. Luhombero

Shirika limetoa elimu kwa wanafunzi na walimu wa shule za Sekondari Inyonga na Ilela; shule za Msingi Inyonga na Kalovya pamoja na maeneo ya wazi, stendi na sokoni wilayani Mlele ambapo muitikio wa uelewa wa elimu hiyo ulikuwa mkubwa
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: