NEMC pamoja na washiriki wengine kutoka Taasisi mbalimbali walioshiriki maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar. Natural Shine Trader wanajishughulisha na vipodozi asili, wanatengeneza sabuni za aina mbalimbali, mafuta ya nywele na massage pamoja na kuchakata mwani na kutoa bidhaa mbalimbali hivyo ameshiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar kwa ajili ya kijitangaza, kutafuta masoko na kujifunza kutoka mataifa yaliyoendelea. TAHA ( Mazao ya mbogamboga, Matunda, Maua na Viungo) wameshiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar kwa ajili ya kuwatafutia wakulima masoko pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania kwenye Sekta ya Kilimo. Johnson Elibarick Kaaya ni mtaalam wa kilimo kutoka Taasisi ya Bodi ya Korosho Tanzania, Bodi ya korosho ni taasisi ya umma iliyoanzishwa chini ya sheria 18 ya mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka 2010 yenye jukumu ya kusimamia tasnia zima ya maendeleo ya zao la korosho nchini Tanzania. Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( CPB) wameshiriki maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar kwa ajili ya kutimiza majukumu yao ya GAPEX ( General Agricultural Produce Export) ambalo ndo jukumu kuu la Bodi katika kutangaza nafaka na mazao mchanganyiko kwenye masoko ya nje. Hapo juu ni Bodi ya Chai wameshiriki maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar kwa ajili ya kutangaza chai ya Tanzania na kutafuta masoko Kituo cha Uwekezaji Tanzania wapo wanatangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Kwetu, wananadi miradi inayotafuta wabia na wanavutia wawekezaji kuja nchini kuwekeza.
Wizara ya Mambo ya Nje kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar ndio waratibu wa ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya tisa ya Kilimo na ya tatu ya Mazingira jijini Doha nchini Qatar. Diana Fatukubonye ni Export Manager kutoka Bodi ya Kahawa (TCB).Bodi ya kahawa ni Shirika la umma lenye mamlaka ya kusimamia tansia ya kahawa nchini Tanzania.Uzalishaji wa kahawa kwa sasahivi ni tani 75,000 ya kahawa safi na tuko kwenye mkakati wa kuongeza uzalishaji kufika tani 300,000 mwaka 2025.
Post A Comment: