Shirika la Umoja wa Kimataifa, umeorodhesha Kenya taifa la 27 kwa orodha ya mataifa yasiyokuwa na furaha. 

Katika ripoti hiyo inayojumuisha mataifa 146, Kenya ilipewa nambari 119, huku UN ikisema kuwa Wakenya waliohojiwa walitaja ufisadi serikalini kama sababu kuu ya wao kukosa furaha. 

Katika utafiti wa mwaka jana uliojumusiha mataifa 149, Kenya ilirodheshwa nambari 28 katika mataifa ambayo raia wake hawana furaha. Kenya (119) imeorodheshwa ya 23 barani Afrika nyuma ya Uganda ambayo inayoongoza Afrika Mashariki kwa raia wake kuwa na furaha, ikiwa katika nafasi ya 117 katika mataifa 146.

Tanzania walichukua nafasi ya 139 huku Uhabeshi maarufu kama Ethiopia ikiwa katika nafasi ya 131. 

Rwanda ndilo taifa ambalo halina furaha zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa mujibu wa utafiit huo. Rwanda ni taifa la nne kutoka chini katika orodha hiyo, juu ya Zimbabwe, Lebanon na Afghanistan. Mauritius ndilo taifa lenya furaha zaidi barani Afrika likichukua nafasi ya 52 ulimwenguni na kufuatwa na Libya, Ivory Coast, Afrika Kusini na Gambia. 

Kwa mwaka wa tano mfululizo, Ufini ilitajwa nchi yenye furaha zaidi ulimwenguni ikifuatwa na Denmark, Iceland, Uswizi na Uholanzi. Ripoti ya Furaha Duniani ilizinduliwa mwaka 2012 na hutathmini furaha ya watu, uwezo wao kiuchumi na kijamii. 



Share To:

Post A Comment: