MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa katikati akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Tanga ambao hawapo pichani kuhusu Tamasha la Utamaduni ( Tanga Utalii Festival) linalotarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii Jijini Tanga kulia ni Meneja wa Bia ya Heineken Kanda ya Kaskazini, Swalehe Madjapa ambao ni mdhamini mkuu wa tamasha hilo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga


MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa katikati akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Tanga ambao hawapo pichani kuhusu Tamasha la Utamaduni ( Tanga Utalii Festival) linalotarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii Jijini Tanga kulia ni Meneja wa Bia ya Heineken Kanda ya Kaskazini, Swalehe Madjapa ambao ni mdhamini mkuu wa tamasha hilo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga
Meneja wa Bia ya Heineken Kanda ya Kaskazini, Swalehe Madjapa ambao ni mdhamini mkuu wa tamasha hilo akizungumza wakati wa mkutano huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa 

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua matukio kwenye mkutano huop

 

NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

TAMASHA la Utamaduni ( Tanga Utalii Festival) linalotarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii Jijini Tanga litatumika pia kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linayotarajiwa kufanyika nchini Agosti mwaka huu ikiwemo kutangaza fursa za utalii, uchumi na utamaduni katika tamasha hilo.

 Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa katika mkutano wake na vyombo vya habari uliofanyika wilayani hapa kuhusu kuelekea Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuwa na aina yake

 Mgandilwa amesema wamekusudia kufanya tamasha hilo kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana mkoani humo pamoja na kutangaza tamaduni mbalimbali za makabila yanayopatikana Tanga.

 "Watanzania moja ya jambo tunalojivunia na tunapaswa kuenzi ni tamaduni zetu,  sisi katika ngazi ya wilaya tumeliona hilo na tumeazimia kufanya tamasha liyakalohusisha tamasuni za watu wa Tanga, hivyo tutakuwa na ngoma mbalimbali," amesema.

Mgandilwa amezitaja ngoma za asili zitakazoshiriki katika tamasha hilo kuwa ni mdumange, baikoko, singeli pamoja na msanja pia kutakuwa na wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya akiwamo Matonya, Kassim Mganga na Dula makabila.

Kwa upande wake Meneja wa Bia ya Heineken Kanda ya Kaskazini, Swalehe Madjapa ambao ni mdhamini mkuu wa tamasha hilo, amesema wameamua kudhamini tamasha hilo kutokana na umuhimu wake kwa watu wa Tanga. 

"Bia ya Heineken tumeona umuhimu wa tamasha hilo katika katika kuutangza Mkoa wa Tanga kimataifa tunaamini kuna fursa nyingi za kiuchumi hivyo tunaamini kupitia tamasha hili tutawavutia wawekezaji," Amesema Swalaehe. 

 Naye Mratibu wa tamasha  hilo,Nasoro Makau ameviasa vyombo vya habari nchini  kuzitangaza nyimbo za asili ili kuendelea kuuenzi utamaduni wa mtanzania. 

 "Vyombo vya habari vinatangaza sana muziki wa kizazi kipya sasa vione umuhimu pia wa kutangaza utamaduni wetu watoto wetu nao watambue kuwa tuna nyimbo zetu za asili wasije wakabobea kwenye tamadunii za kimagharibi na kuacha tamaduni zao.

 

"Tamasha litakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo mbio fupi, burudani kutoka kwa wasanii tofauti kwa hiyo kwa wenyeji wa Tanga tunawasihi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Jengo la Urithi, tamasha  litaanza saa 12 asubuhi na halina kiingilio.  Kauli mbiu ya tamasha hilo ni 'Tanga Festival, karibu mahabani," amesema.

 

Mwisho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: