Akizungumza katika mafunzi hayo Salum Nyangwese Afisa Uchunguzi kutoka Takukuru ameeleza kuwa mazingira ya rushwa hutengenezwa na Wafanyakazi wasio waadilifu kazini Kwa kuchelewesha maamuzi na kuweka urasimu katika kutoa huduma na utekelezaji wa majukumu yao ya msingi na hivyo kuwataka Wafanyakazi wote kurejea katika majukumu yao ya kazi kama sheria za ajira zinavyoelekeza ili kuweza kufanya maamuzi Kwa wakati na uaminifu ili kuweza kuzuia mianya ya rushwa.
Kwa upande wake mwanasheria wa Takukuru Mkoa wa Arusha Violet machary amewataka Wafanyakazi hao kuzingatia mafunzo hayo ambayo hutolewa Kila mara ili kufanya kazi kwa weledi na umakini katika utekelezaji wa majukumu yao ya Kazi.
Nao baadhi ya Wafanyakazi wa Chuo hicho wamekiri kuwa mafunzo hayo ambayo hufanyika Kila mara chuoni hapo yamewajengea uwezo na uelewa mkubwa hasa katika kutambua vitendo vya rushwa na Uhujumu uchumi na kuomba mazingira ya utendaji kazi kwa Watumishi wa umma nchini Kwa kuboreshewa mazingira ya kazi.
Post A Comment: