Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya Sisi Tanzania Mkoa wa Singida imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza Mwaka Mmoja wa Uongozi wake tangu alipoingia madarakani.
Akizungumza wakati wa kutoa pongezi hizo katika kikao cha viongozi wa Taasisi hiyo kilicho keti leo Ukumbi wa Kanisa la Romani Katoliki (Social) mjini hapa , Mratibu Msaidizi wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida Yahaya Njiku alisema Watanzania wanakila sababu ya kumpongeza Rais Samoa Suluhu kutokana na uongozi wake uliotukuka.
"Katika kipindi cha mwaka mmoja tangu awe madarakani Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha uwezo mkubwa wa kuongoza nchi kwani amefanya mambo mengi ambayo Watanzania hawakuyategemea" alisema Njiku.
Alisema Taasisi hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada zake zote za kuongoza nchi na kuwaletea maendeleo Wananchi wa Tanzania.
Wakati huohuo Mweka Hazina wa
Taasisi hiyo Omary Hamisi amewataka vijana mkoani hapa kuendeleza kudumisha amani na utulivu wa nchi
ambao tumeachiwa na waasisi wa taifa letu Hayati Julius Kambarage Nyerere na
wenzake.
"Vijana ni kundi kubwa ambalo linatakiwa kwa nguvu moja kuitunza
amani na utulivu wa nchi yetu hivyo tuna kila sababu ya kufanya hivyo"
alisema.
Alisema Taasisi hiyo malengo yake makubwa ni kuisaidia serikali
katika shughuli mbalimbali za maendeleo
na kutekeleza mambo mbalimbali yanayowagusa vijana.
Mratibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida Shabani Mukee alisema kikao hicho
kiliketi kwa ajili ya kujadili ajenda kadhaa ikiwemo ya kuandaa kongamano la
uzinduzi wa taasisi hiyo, kuwa na sare za taasisi na kumpongeza Rais Samia
Suluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja wa kuwa madarakani ambapo amefanya kazi
kubwa katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Mukee alitaja mambo mengine yaliyojiri kwenye kikao hicho kuwa ni
ufunguzi wa kikao, utambulisho, kutoa taarifa ya utambulisho wa taasisi hiyo kutoka
kwa mkuu wa mkoa na taasisi kuwa na
ofisi ya mkoa.
Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wote kutoka wilaya zote za Singida ambazo ni Iramba, Itigi, Mkalama, Manyoni, Ikungi, Singida Mjini na Singida DC.
Post A Comment: