Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akionesha moja ya zao la alizeti wakati alipotembelea mashamba ya wakulima katika Kata ya Mudida Halmashauri ya Singida Vijijini wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja aliyoifanya jana.

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge na Diwani wa Kata ya Mudida Omari Mande wakiangalia jinsi baadhi ya majani ya zao la alizeti yalivyoshambuliwa na wadudu wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Vijijini Mhandisi Paskas Muragili akizungumza katika ziara hiyo. Kulia ni Afisa Mtendaji Kata ya Mudida, Faraja Yona 
Muonekano wa mashamba ya alizeti katika Kata ya Mudida.
Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akionesha moja ya zao la alizeti wakati alipotembelea mashamba ya wakulima katika Kata ya Mudida Halmashauri ya Singida Vijijini wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja aliyoifanya jana.

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge na Diwani wa Kata ya Mudida Omari Mande wakiangalia jinsi baadhi ya majani ya zao la alizeti yalivyoshambuliwa na wadudu wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Vijijini Mhandisi Paskas Muragili akizungumza katika ziara hiyo. Kulia ni Afisa Mtendaji Kata ya Mudida, Faraja Yona.
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Singida Vijijini, Nathalia Moshi akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
Ukaguzi wa mashamba hayo ukiendelea.

Ukaguzi wa mashamba hayo ukiendelea. Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata hiyo Omari Mande, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge na Mkulima wa Kata ya Mudida, Fr Pasian Mwanga -Paroko Parokia ya Mtinko.


Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge amesema wanatarajia kuitisha mkutano utaowakutanisha wadau wote wa zao la alizeti na wakulima kwa ajili ya kupanga bei ilikuwaondelea wakulima changamoto ya kuuza zao hilo wakati msimu wa mauzo utakapo wadia.

Dk. Mahenge aliyasema hayo wakati alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kutembelea mashamba ya wakulima ya  zao hilo  katika Kata ya Mudida iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini.

Alisema Mkoa wa Singida katika msimu huu wa kilimo wa 2021/2022  unategemea kuvuna tani 580,000 za alizeti ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara tatu ikilinganishwa na msimu uliopita na hiyo imetokana na uhamasishaji wa wadau wa zao hilo  na ukopeshwaji wa  mbegu  zenye ruzuku ya Serikali  kwa wakulima.

Alisema kazi hiyo kubwa ya kuongeza zao hilo imetokana na makampuni mbalimbali kuwakopesha mbegu hizo wakulima na kuwa lengo la Serikali limefanikiwa kwa kiasi kubwa  jambo litakalo saidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kula ambayo yalikuwa yakiagizwa kutoka nje ya nchi.

"Kufuatia ongezeko hilo ni lazima tufanye mkutano na wadau wote wa kupanga bei yenye tija ili mkulima asipunjike kwani bila ya kufanya hivyo wanaweza kutokea wajanja wakaanza kununua zao hilo kwa bei ndogo na kumuangusha mkulima" alisema Mahenge.

Alisema muitikio wa wakulima wadogo na wakubwa wa kutumia mbegu hizo za ruzuku zilizotolewa na Serikali zimeleta tija na kutoa mavuno mengi msimu huu.  

Dk. Mahenge alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wakulima na wadau mbalimbali wa zao hilo yakiwemo mashirika na makampuni mbalimbali yaliyojitolea kulima na kuwasaidia wakulima kupata mbegu baada ya ile iliyokuwa inatarajiwa kutoka izara ya Kilimo kutokidhi mahitaji. 

 Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Paskas Muragili alisema kwamba pamoja na kutofikia malengo ya kupata mbegu  za kutosha wananchi na mashirika mbalimbali waliweza kuweka jitihada za upatikanaji wa mbegu kwa kununua sehemu mbalimbali jambo ambalo limesaidia kuongeza uzalishaji na kufanya wavuke malengo.

“Tangu wananchi wa Singida waanze kulima zao ili  hawajawahi kulima mashamba makubwa kwa ufanisi kama kipindi hiki, na hii imetokana na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na serikali pamoja na ugawaji wa mbegu kwa mkopo. Singida tutavuna alizeti nyingi kuliko miaka yote” alisema  Muragili. 

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Stanslaus Choaji  alisema Mkoa wa Singida ulipata  mbegu za alizeti  tani 469 kwa ajili ya kupanda ekari  239,700 jambo ambalo lilitekelezwa.

Alisema malengo ya mkoa ilikuwa ni kupata mbegu za alizeti tani 581.9 ambazo zingeweza kuwatosheleza wakulima wote na badala yake wakapata kiasi cha tani 469 ambazo hazikuweza kukidhi mahitaji ya wakulima wote.

Alisema Wilaya ya Singida Vijijini ilipata  mbegu  za alizeti tani 76.04 kutoka kwa Wakala wa Mbegu  nchini (ASA)  kupitia Wizara ya Kilimo ambazo zilisambazwa katika kata 21 za wilaya hiyo ambapo pia  ilipata tani 3.8 za alizeti zilizotolewa na Shirika la IFARD ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo na kuondoa changamoto ya upungufu wa mafuta ya kupikia hapa nchini.

 Choaji alisema kutokana na mwitikio mkubwa wa wakulima pamoja na kwamba walipata mbegu pungufu lakini matokeo yatakuwa makubwa kwa kuvuka malengo ya kiasi walichotegemea kuzalisha.

Akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Singida, Afisa Kilimo wa wilaya hiyo Nathalia Mosha alisema Halmashauri hiyo ina eneo linalofaa kwa kilimo lipatalo hekta 321,400  ambapo  3, 400 zinafaa kilimo cha umwagiliaji.

Alisema katika msimu wa kilimo wa 2021/2022 wamelima hekta 38,936 na matarajio ni kuvuna tani 73,936 ambapo mbegu za alizeti zilizotumika ni standard seed, Hysun 33, supersun 66 na recod zilizozalishwa na wakulima wenyewe.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: