Na Ahmed Mahmoud
SERIKALI imetakiwa kuwekeza nguvu kubwa na kutatua changamoto katika Eneo la ubunifu, ili kupiga hatua kwenye Sayansi na Teknolojia, itakayosaidia nchi kufikia maendeleo endelevu.
Kwa muktadha huo nchi kupiga hatua ya maendeleo ya kiuchumi,katika kilimo katika Zao la Parachichi itakayosaidia kuongeza wigo mpana,wa kuzalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika kimataifa.
Wabunifu nchini wamekuwa na changamoto kadhaa wa kadhaa, Jambo linalopekea kutofikiwa kwa malengo yao,kwa msaada wa serikali hivyo ni muda Sasa kuweza kutazama eneo hilo.
Wanahabari na watafiti wa kanda ya kaskazini waliopatiwa mafunzo ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) walijionea teknolojia mbalimbali za utafiti uliofanywa na watafiti wetu sanjari na wabunifu.
Makala haya yatajikita zaidi kuangazia eneo la ubunifu ambapo tutawaangalia wabunifu kikundi cha AVOMERU GROUP ambao wamekuja na utengenezaji wa mafuta yatokanayo na Zao la Parachichi na kuwezesha vikundi kadhaa kujikwamua kiuchumi.
Waandishi hao na watafiti walipata nafasi ya kuelezwa kwamba kumekuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya baridi,masoko ya mazao Mafuta hayo,ambayo yapo katika nchi za Asia,lakini kutokana na usafirishaji wa mizigo,inabidi mawakala wawepo nchi jirani ya Kenya.
Kwa kipindi kirefu Sasa watafiti wetu wameendelea kutoa tafiti kadhaa zenye kueleza na kubuni masuala mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa kimaendeleo na kuendana na masoko ya kimataifa.
Akielezea katika ziara ya mafunzo kwa wanahabari Jesse Avojange Mkurugenzi wa Avomeru Group anasema kwamba taasisi hiyo ilianza rasmi Mwaka 2017 katika kuongeza thamani ya zao la Parachichi ila Mwaka 2015 ndio wakaanza kushirikiana na COSTECH kuzalisha mashine za kuchakata zao hilo.
Anaeleza kwamba walianza kutengeneza mashine za mfano Lengo lao likiwa ni kuzalisha mafuta ya Parachichi kwa kuvitumia vikundi huko vijijini mikoa ambayo inazalisha zao hilo.
Anasema kwamba baada ya kupata Fedha za kuendeleza Ubunifu kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ndipo Mwaka 2017 walianza rasmi na vikundi vya wakulima kwa kuwafungia mashine kuzalisha mafuta hayo.
Kwa mujibu wa Avojange Baada ya kuwapa wakulima mashine wanaendelea kufanya utafiti wa mashine hizo na kuanza kuwapelekea na kuwafundisha jinsi ya uchakataji wa mafuta hayo.
Anabaisha kwamba baada ya kujua jinsi ya uzalishaji wa mafuta vikundi hivyo huongezewa ujuzi wa kuzalisha kwa ubora unaokubalika katika Masoko ya kimataifa ili kutoa mafuta yenye ubora unaokubalika.
Anasema kwamba uzalishaji wa mafuta pia waligundua kuna fursa nyingi za bidhaa zinazotokana na Zao la Parachichi ikiwemo mbegu zake wakaanza kuzalisha unga wake pia kuziotesha kwa mbegu zinazokubalika katika masoko ya kimataifa na hapa nchi ili yasiharibike.
"Tulianza kuwafundisha wakulima Teknolojia mpya ya kuotesha mbegu za Parachichi ili kuondokana na Zao hilo kuharibika ndani ya muda mfupi hivyo tunawafundisha wakulima jinsi ya kupandisha mbegu za zao hilo ili kutoa mazao kwa muda mfupi"
"Mbegu za Parachichi tulianza kuzalisha Unga wake tukizani itakuwa mbadala wa majani ya chai na Kahawa tukaona muitikio mkubwa wa watu waliokubali kulima zao hili ndio tukaanza uzalishaji wa mbegu za muda mfupi"anaeleza.
Anaeleza kwamba tokea Mwaka 2017 hadi Marchi Mwaka huu wameotesha Miche 100,3010 ya Zao la Parachichi nchini na wanaigawa kwa wakulima kulingana na ukubwa waeneo Miche kwa idadi inayolingana.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wamekuwa wakiingiza wakulima katika kanzidata yao baada ya kuwapa miche ili kubaini ukuaji na uzalishaji utaanza lini kwa Mwaka Jana wametoa tani 1600 ya Miparachichi waliowapa wakulima hao.
Anasema mti wa mparachchi kuanzia kupandwa hadi kukua una uwezo wa kutoa kilo 40 hadi 50 kwa Mwaka wa kwanza ila miaka inayofuata inatoa Mara mbili ya Mwaka wa kwanza kilo 80 au 100 na kuongeza uzalishaji.
"Hizi ni faida zinazotokana na Zao hili kwa wakulima kuongeza uzalishaji na kupata faida kutoka debe tsh.2500 na upotezaji wa zao hilo ambalo halihimili muda mrefu" Anaeleza Avojange.
Hivi karibuni hapa nchini hususani mikoa ya kanda ya kaskazini na ukanda wa Kusini katika mikoa ya Mbeya Iringa na Ruvuma wameanza uzalishaji wa miche ya kisasa ya Parachichi na kupelekwa nje ya nchi ambapo zao hilo pia linafaida nyingi kwa mwili wa binadamu ikiwemo mafuta yake.
Ambapo yanaelezwa wekwamba yanafaa Sana kwa upikaji wa chakula na bora kuliko mafuta mengine ya kula hivyo watumiaji changamkieni na serikali iwezeshe kuchakata mafuta haya hapa nchini.
Post A Comment: