Na,Jusline Marco:Arusha


Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania na Afisa Mtendaji wa Shirika la TAHA Dkt.Jacqueline Mkindi amezipongeza sekta binafsi kwa ushiriki wao katika maonesho ya kimataifa ya kilimo (TANZ FOOD ) yaliyofanyika jijini Arusha


Akizungumza katika maonesho hayo ambayo yamefanyika katika viwanja vya magereza Kisongo jijini humo,Bi.Jacqline amesema sekta ya kilimo ndiyo sekta ambayo inashikilia mhimili wa uchumi nchini kupitia masoko ya kimataifa


Aidha amesema nchi nyingi barani Afrika zinahitaji bidhaa kutoka Tanzania hivyo maonesho  hayo yanatoa fursa na chachu kwa watanzania hasa wa sekta binafsi katika kujifunza zaidi.


"Kujifunza ni muhimu ili kuendelea kiongeza tija kwenye uzalishaji na usindikaji wa bidhaa mbalimbali."alisema mwenyekiti huyo wa baraza la kilimo Tanzania


Vilevile Dkt.Jacqueline ameongeza kuwa pamoja na maonesho hayo washiriki watapata fursa ya kubadilishana mawazo na taarifa muhimu ili kuweza kuyafikia masoko ambapo amewahakikishia watanzania kuwa fursa zilizopo katika sekta ya kilimo katika mazao ya mbogamboga na matunda.


"Dunia inahitaji matunda ,mbogamboga na viungo kutoka Tanzania kwahiyo niwahamasishe watanzania wenzangu tuwekeze kwenye kilimo lakini tuwekeze kwa akili huku tukitafuta taarifa muhimu na kuona ni jinsi gani tutaendelea kujengeana uwezo wa ndani ili tuweze kushindana kimataifa."alisema Dkt.Jacqueline


Sambamba na hayo ameeleza kuwa kwa sasa Shirika la TAHA linafanya kazi kwenye mikoa 26 huku vijana na akina mama wakionekena kujitokeza kwa wingi katika kilimo cha mazao ya Horticulture ambapo amewataka vijana kujikita katika kilimo biashara cha mbogamboga na matunda.

Share To:

Post A Comment: