Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga akipokea agizo kutoka kwa Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango juu ya Jeshi la Polisi mkoani hapo walivyotuhumiwa kupiga wananchi mara wanapokua wamekamatwa katika matukio mbalimbali katika jamii likiwepo la kusumbuliwa katika mgogoro wa baina ya wananchi na mwekezaji Manyara Estate.

 Na Mary Margwe, Babati


Jeshi la Polisi Mkonia Manyara limeonywa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi za kuwapiga wananchi pale wanapokua wamepatwa na tuhuma za kukamatwa kutokana na matukio mbalimbali katika jamii na hivyo amemtaka kamanda wa Polisi Mkoani hapo Benjamin Kuzaga kuhakikisha analidhibiti hilo lisijirudie tena.

Hayo yalibainishwa juzi na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango wakati alipokua akifungua daraja la Magara wilayani Babati Mkoani Manyara mbele ya mkuu wa mkoa wake Makongoro Nyerere, ambapo alisema kufanya hivyo kutasaidia kudumisha upendo na amani katika jamii, ambapo alisema ataki tena kusikia wananchi wanapigwa.

Dk. Mpango alisema hayo kufuatia mamamiko yaliyotolewa na diwani wa Kata ya Magara wilayani Babati Mkoani Manyara Jacob Elias kuwa Polisi wamekua wakiwapiga na kuwajeruhi vikali wananchi mara wanapokua wamekamatwa kutokana na tuhuma mbalimbali likiwepo la wananchi kusumbuliwa kwenye ule mgogoro wa wananchi na mwekezaji wa Manyara Estate lilikokuwepo km. 1 kutoa daraja la Magara.

Aidha alisema hakuna yeyote mwenye mamlaka ya kupiga wananchi, yeyote yule ahakikishe anafuata taratibu za kiserikali zipo na sio kujichukulia sheria mikononi kama ambavyo diwani ameeleza hapo, huku alisema hakuna kwenye mamlaka ya kupiga wananchi.

Kufuatia hilo alimtaka kamanda wa Polisi Mkoa huo Benjamin Kuzaga kuhakikisha anamtolea taarifa kwa hao Polisi wanaotuhumiwa kutenda kitendo hiko cha kikatili na kumuonya vikali ili kuacha mara moja hivyo kitendo, vyombo vya kisheria vipo wavitumie.

" Nimemsikia diwani, hao wanaopiga wananchi, RPC yupo, RPC sitaki tena kusikia kwamba wananchi wetu wanapigwa, yeyote yuleafuate taratibu za kiserikali zipo, hakuna kwenye mamlaka ya kupiga wananchi wetu" alisema Dk.Mpango.

" Kwahiyo mnitolee taarifa viongozi wetu wapo, na mkamuonye, mwambieni Makamunwa Rais katika vitu ambavyo alikasirika sana moja ni hili, watu wazuri kabisa sura zao zinapendeza angalia vijana hawa" alikemea Dk. Mpango.

Aidha Dk.Mpango alisema Tanzania ambayo wameirithi kwa waasisi wa Taifa hilo, kuwa ni Taifa lenye amani , hivyo amewataka wananchi kuishi kwa amani na upendo, migogoro imekuwepo kati ya wanadamu, isipokua hawapaswi kujichukulia sheria mikononi kuanza kukatana katana mapanga, huko ni kwenda kinyume na taratibu, sheria na kanuni za nchi.

" Tunakaa kwa amani na upendo, na serikali ipo kuanziavhini kabisa hwahiyo nataka kuwasihi migogoro imekuwepo kati ya wanadamu, lakini msijichukulie sheria mikononi kuanza kukatana katana mapanga wala nini, panapoua na mfikishe kwenye vya serikali,waambieni viongozi wa chama wako hapa ilitumalize migogoro kwa amani" aliongeza Dk. Mpango.

Mbali na hilo amewataka wakazi wa eneo la daraja la Magara kuhakikisha wanakua walinzi wa hilo daraja, na kwa hilo amesema hakuna atakayefumbiwa macho, na yule atakayedhani wanafanya mchezo asifanye mchezo na hela ya mama.

"Tumepata chombo kizuri hapa kwa maana ya daraja la Magara, mkiendelea kulima vibaya vibaya mto huu utahama na kupotea, hivyo tutunze mazingira hili tulizingatie, lakini lazimatutunze mazingira yetu ili nayo yatutunze" aliongeza Dk. Mpango
Share To:

Post A Comment: