Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela kushoto akimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Ruby International Ltd na Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe. Salim Alaudin Hasham wakati wa ziara yake alipofanya ziara katika migodi ya Epanko wilayani Ulanga kwa lengo la kujionea namna shughuli za uchimbaji madini unavyofanyika.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela kulia akiwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Ruby International Ltd na Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe. Salim Alaudin Hasham aliyesimama katikati wakati wa ziara hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amempongeza Mkurugenzi wa kampuni ya Ruby International Ltd na Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe. Salim Alaudin Hasham kwa kampuni yake kuwa kinara wa ulipaji kodi katika sekta ya madini.
Shigela
ameyasema hayo wakati alipofanya ziara katika migodi ya Epanko wilayani
Ulanga kwa lengo la kujionea namna shughuli za uchimbaji madini
unavyofanyika.
Aidha
Shigela alipata wasaa wa kuzungumza na wafanyakazi wa migodi hiyo huku
akiwasihi kuwa waaminifu ili kumpa nguvu mwekezaji huyo mzawa aendelee
kutanua wigo wa uwekezaji na ajira ziweze kuongezeka.
Kwa
Upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ruby International ltd na Mbunge
wa Jimbo hilo la Ulanga amesema anajivunia kuwa ni sehemu ya kuzalisha
ajira kwani kwasasa anawafanyakazi zaidi ya 300 na anatarajia kutanua
mgodi huo ili aweze kufikia ajira 700 mpaka 1000.
Migodi ya Epanko inachimba madini ya Spinel ambayo yanatumika kutengenezea thamani mbalimbali.
Mkuu
wa mkoa Martine Shigela yupo wilayani Ulanga kwa ziara ya siku mbili
kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo inavyokwenda na kuhakikisha
fedha za serikali zinatumika ipasavyo.
Ruby International Ltd iliibuka kinara wa ulipaji kodi katika sekta ya
Madini na kukabidhiwa tuzo iliyoandaliwa na wizara ya madini katika
hafla maalum ambayo Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete alikuwa mgeni rasmi.
Post A Comment: