Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maji Pamela Temu akizungumza wakati wa Jukwaa hilo |
Mkurugenzi wa Bonde la Maji Pangani Segule
Segule akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mkutano huo |
MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo akizungumza wakati wa Jukwaa hilo |
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakufuatilia matukio
NA OSCAR ASSENGA,MUHEZA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ameziagiza Halmashauri za mkoa huo kutengeneza sheria za ndogo ambazo zitalinda mazingira na vyanzo vya maji ikiwemo kuwataka kutokuruhusu watu kuvichezea .
Malima aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Wadau Bonde la Mto Pangani ambalo limefanyika Jijini Tanga ambapo alisema lazima wahakikishe wanakuwa wakali sana kwani mambo mazuri hayataki kubembelezana
Alisema pia suala la mazingira na maji ni kama vile uji na mgonjwa hivyo ukiwaona watu wanachafua vyanzo vya maji kwa kutia zebaki kwenye vyanzo vya maji na kuvichafua lazima wachukuliwe hatua kali za kisheria.
“Suala la Mazingira na Maji ni kama vile uji na mgonjwa hivyo ukiona watu wana weka zebaki kwenye vyanzo vya maji halafu anasimama mbele za watu anasema hao wanapiga kelele bure yeye anachangua mapato kwenye Halamshauri sio sawa chukueni hatua “Alisema
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa sababu mtu huyo atakuwa anachangia magonjwa kwa watumiaji wa maji na jumuiya zenu hivyo wawe wakali kwa wachafunzi wa vyanzo vya maji kuhakikisha wanazibiti .
“Ndugu zangu wadau wa Jukwaa hili kuweni wakali kwenye vyanzo vya maji msikubali watu waingie wachezee hakuna cha Tanga,Arusha wala Moshi mkifanya masishara vyanzo vitakauka heshimuni masharti ya matumizi ya maji yaliyopo kwa kila mmoja”Alisema
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba watu wakifanya mchezo kwenye vyanzo vya maji vinaweza kukauka na hivyo kupelekea changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa maisha
“Ndio maana tumeamua kuanzisha Jukwaa hilo tujadili lakini ukichezea vyanzo vya maji mito itakauka kuna miradi ya maji watu wanapiga sana lakini tunamshukuru Rais Samia Suluhu miradi ya maji imeinginia heshima kubwa kutokana na usimamizi mzuri”Alisema
“Mkiona mradi wa maji hauna maelezo na kila mwaka unaambiwa unaishi lakini hauishi ukimuangalia mkandarasi kanawiri,wakina mama wana beba maji hii sio sawa mradi wa maji lengo lake ni kutoa maji”Alisema
Hata hivyo amelipongeza Bonde la Pangani kwa kuwashirikisha wadau kwenye rasiliamali za maji na kuimarisha jumuiya za watumiaji wa maji huku akiwataka waendelee kufanya jitihada za makusudi kutunza vyanzo vya maji.
“Lakini muelewe kwamba hakuna mtu mahususi mwenye dhamana ya usimamizi wa maji ukiona mtu anachafua vyanzo vya maji ukasirike muwafichue msiwafumbie macho”Alisema RC Malima.
Awali akizungumza wakati wa Jukwaa hilo Mkurugenzi wa Bonde la Maji Pangani Segule Segule alisema bonde la linahusisha ukubwa wa kilomita 58600 katika mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Tanga na sehemu Manyara,
Alisema kazi kubwa ni kuhakikisha rasilimali za maji zinatunzwa ipasavyo na kusimamia vyanzo kwa kuhakikisha wanafanya shughuli za urudishaji uoto asili katika vya vyanzo vya maji ikiwemo upandaji miti,kutumia njia mbalimbali kupelekea uelewa kwa jamii na wananchi.
Alisema lengo la Jukwaa hilo la wadau ni kujadiliana kuhusu rasilimali za maji changamoto za vyanzo na kukabiliana nazo kwa kuchukua ili kuweza kukabiliana nazo.
“Changamoto za bonde ni ya watu wa madini kuchimba madini kwenye vyanzo vya maji maeneo ya Lushoto Muheza lakini pia ukataji wa miti kwenye eneo la hifadhi,uchafuzi vyanzo watu kutupa taka kwenye vyanzo vya maji kugeuza vyanzo vya maji kuwa sehemu uya kutupia taka”Alisema
Mwisho.
Post A Comment: