Na Ahmed Mahmoud
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Marry Masanja amewaongoza zaidi ya wanawake 500 kwenda kutembelea mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambapo pia ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Akizungumza wakati wakianza safari hiyo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Masanja amesema kwamba tukio hilo ni kuunga mkono juhudi alizoanza Rais Samia Suluhu Hassan ambapo alisema wamechagua wiki hii ya wanawake Duniani kuionyesha Afrika na Dunia kwa ujumla na kuwakumbusha watanzania kwamba wao ni wajenzi wa taifa lao.
“Na kujenga kwetu ni kwa vitendo ambapo tunapoenda kuona vivutio sio kwa kutazama tuu lakini pia kwa kujifunza kwani Kuna mambo mengi ya kujifunza vikiwemo viumbe hai pamoja na fuvu la mwanadamu wa kwanza ambalo huwezi kulikuta sehemu yoyote Duniani,amesema Masanja.
Amefafanua kuwa wanaamini Ngorongoro ni bustani ya Eden hivyo wameona katika maadhimisho ya siku ya wanawake hawawezi kukosa kwenda ambapo pia Alieleza kuwa suala la kukuza utalii wa ndani linaanza na mtu mmoja mmoja lakini pia ni sehemu ya kutekeleza na kuunga mkono juhudi za Mh.Rais wetu ambaye amekuwa mshiriki namba moja wa kutangaza utalii wetu.
“Nifuraha kubwa kuona kundi hili la kinamama waliojitokeza kuunga mkono suala zima la kukuza utalii wa ndani na wanawake wanaweza kuukuza utalii wa ndani na waneonyesha kwa vitendo kwa kulipa fedha zao kutembelea hifadhi ya Ngorongoro”amesema.
Awali akizungumza katika tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amesema kuwa Tanzania imefunguka,Arusha imefunguka,mh.samia kazi iendelee.
Amesema kuwa, serikali ipo pamoja nao ikiwa ni siku ya pili ya juma la maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inayokwenda sambamba na tukio hilo la uhamasishaji wa utalii wa ndani wote karibuni Arusha.
Kwa upande wake Balozi wa utalii wa jumuiya ya Afrika Mashariki Sharon Ringo amesema kuwa anayofuraha kubwa sana ya kuwa sehemu ya kuutangaza utalii wa ndani kwenda kujionea kivutio na Eden.
Aidha amesema kwamba sio wanaume pekee yao wanaweza kufanyakazi hata wanawake wanaweza nazikawa msaada mkubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Home
Unlabelled
NCAA YAPOKEA WANAWAKE ZAIDI YA 500 KUKUZA UTALII WA NDANI
Post A Comment: