Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew(Mb) amewataka wakazi
maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kushiriki kikamilfu katika zoezi utekelezaji mfumo wa Anwani za Makazi
pamoja na Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwezi Agosti 2022
Mheshimiwa Mhandisi Kundo ameyasema hayo jana Alhamisi, Machi 10, 2022 Wilayani ya Bariadi Mkoa wa Simiyu
alipofanya ziara katika vijiji mbalimbali vya Wilayani humo ya kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa Anwani za Makazi
naotakiwa kukamiliza ifikapo mwezi Mei 2022.
Alisema kuwa wananchi wote wanaoshi katika Wilaya ya Bariadi wakashiriki kikamilifu katika
utekelezaji mfumo wa Anwani za Makazi ili ukawe rahisi kwenda kutekeleza zoezi la
Sensa ya watu na makazi litakalofanyika mwezi Agosti, 2022 ambalo litapelekea urahisi wa ufikishwaji wa huduma na
maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo kuendana na idadi yao
Nae Mkurugenzi wa Huduma za Posta wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Caroline Kanuti
alitumia fursa hiyo kuwaelezea wakazi wa Manisapaa ya Bariadi umuhimu wa mfumo wa Anwani za makazi endapo
watashiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
“Pale ulipo unaweza ukapata tatizo, unauguliwa au nyumba imewaka moto au kuna mgonjwa anataka kupelekwa hospitali
unapiga simu unajitambulisha tu kwamba nipo kitongoji fulani unataja na namba ya nyumab yako kisha yule unaempigia
simu atakuja mapka pale ulipo kwahiyo kupitia mfumo wa Anwani za makazi inakuwa rahisi kupata msaada”.
Alisema kuwa mfumo wa Anwani za Makazi unarahisisha shughuli za mbalimbali ikiwemo za kilimo kwa
kununua mazao au pembejeo za kilimo popote ulipo na bidhaa yako kukufikia kwa urahisi.
Post A Comment: