Na,Jusline Marco:Arusha


Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha imekabidhi miradi ya ujenzi wa madarasa iliyokuwa ikitekelezwa ndani ya halmadhauri ya jiji la Arusha kipitia fedha za UVIKO 19 kwa wananchi wa jiji hilo na kuwasihi kuitunza miundombinu hiyo.

Akikabidhi miradi hiyo kwa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Said Mtanda amesema kupitia fedha za UVIKO 19 zimeiwezesha jiji la Arusha kujenga madarasa 105 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.1,vyoo 44  pamoja na madawati 5250 .

Aidha Mtanda amesema kwa mahitaji yaliyobaki wanakwenda kujipanga ili kuhakikisha uhitaji wa madarasa na madawati katika shule zote za jiji la Arusha wanakamilisha ambapo amesema serikali ya wilaya inathamini kazi zinazofanywa na walimu ambazo zimelifanya jiji la Arusha kushika namba 1 katika mitihani ya kitaifa kwa miaka 5 mfululizo kwa shule za msingi na katika sekondari wamekuwa katika matokeo ya juu.

"Ufaulu huu unachangiqa na motisha kwa walimu lakini pia chakula kwa wanafunzi mashuleni kitu ambacho tunaendelea kukiwekea mkazo."alisema Said Mtanda Mkuu wa Wilaya ya Arusha

Vilevile amesema Wilaya imetenga kiasi cha shilingi milioni 81 kwa ajili ya mkutano wa walimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na wadau wa elimu ambao wanajitolea kuhakikisha jiji la Arusha linashika nafasi ya kwanza kitaifa kutaofanyika hivi karibuni jijini Arusha.

Akipokea miradi hiyo na kuikabidhi kwa wananchi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Bwn.Joseph Massawe amewataka wazazi na walimu kwa kushirikiana na wanafunzi wao kuhakikisha wanalinda na kutunza madarasa hayo.

Naye Mjunbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Dkt. Daniel Palangyo amepongeza juhudi za usimamizi wa miradi hiyo zinazofanywa na wasaidizi wa Mhe.Rais Samia na kusema kuwa Mkoa wa Arusha umemuelewa kwa vitendo Mhe.Rais kupitia miradi inayotekelezwa.

Aidha amewataka viongozi ngazi ya Mkoa,Wiaya,Halmashauri pamoja na wenyeviti wa mitaa kuendelea kusimamia miradi hiyo sambamba na kuwaambia wananchi kazi zinazofanywa na serikali yao.

"Tuwapongeze sana wana arusha kwa kuona jitihada hizi ,tuendelee kumuunga mkono Rais wetu na serikali yake ili mazuri zaidi yaendelee kuja."alisisitiza Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho

Naye Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Arusha Mussa Matoroka amesema utekelezaji wa miradi ndani ya jiji la Arusha imegharimu jumla ya fedha shilingi bilioni 2.1,fedha zitokanazo na uviko.

Kwa upande Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewapongeza walimu hao kwa jitihada zao za kuhakikisha wanatekeleza agenda iliyopo ya kufanya vizuri kwenye mtihani taifa wa darasa la 4 na darasa la 7 kuwa wa 1 katika elimu ya msingi na katika elimu ya sekondari kuwa wa 1ambapo amewataka kuzidi kushirikiana.

Wakitoa taarifa za utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo wakuu wa shule za sekondari ambazo miradi hiyo imetekelezwa wamesema kuwa ukamikaji wa miradi hiyo kumeondoa changamoto ua msongamano wa wanafunzi madarasani ambapo wameshukuru Mhe.Rais Samia kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo katika shule zao kipitia fedha za UVIKO 19.


Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha pamoja na viongozi wa Serikali ya Mkoa na Wilaya,ikiwasili katika moja ya miradi ya ujenzi wa madaraja yaliyojengwa kwa fedha sa UVIKO 19 ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha.


Moja ya miradi ya ujenzi wa madarasa inayojengwa kupitia fedha za UVIKO 19 ambayo imetembelewa na kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Arusha.


Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Saidi Mtanda akikabidhi miradi ya ujenzi wa madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO 19 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Ndg.Joseph Massawe kwenye ziara ya kamati ya chama hicho iliyofanyika katika Halmashauribya jiji la Arusha.



Mradi wa ujenzi wa madarasa kupitia fedha za UVIKO 19 katika shule ya Sekondari Themi ukiwa umekamilika kwa asilimia 100 ambapo miradi hiyo ometekelezwa pia katika shule nyingine imepunguza changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akiwapongeza watendaji kwa usimamizi mzuri wa miradi ya ujenzi wa madarasa,katoka ziara ya kamati ya siasa ya ccm Mkoa wa Arusha.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Mussa Matoroka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kamati ya chama hicho katika miradi ya ujenzi wa madarasa iliyo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha.
Share To:

JUSLINE

Post A Comment: