Kutokana na kuwepo kwa taarifa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Mwenyekiti wa TLP Taifa Augostino Mrema ,hatimaye Halima amevunja ukimya kuhusu ndoa yake na Mwenyekiti huyo kwamba hana ugomvi na familia yake na watu waache uzushi wa kumzushia kwamba mumewe huyo mtarajiwa amepata upinzani mkubwa kumuoa yeye .
Amesema kuwa,hana mgogoro wowote na mpenzi wake mtarajiwa wananchi wapuuze maneno yanayo sambazwa mtandaoni kwamba yeye na mzee wana mgogoro sio kweli,bali familia wanaishi nao vizuri na wala hakuna neno na ameshapewa baraka zote amsaidie baba yao.
Halima amesema swala la ndoa yake kufungwa siku ya alhamisi bado ni mapema sana kusema kwani kipindi hiki ni cha kwaresma hivyo muda ukifika watasema jambo lao ni lini lakini kwa sasa hayupo tayari kusema mambo mengi isitoshe yeye sio mwana siasa .
Mmoja wa watoto wa mzee Mrema ambaye jina limehifadhiwa amesema kuwa , hawana mgogoro wowote na baba yao kuhusu kuoa kwani mzee Mrema ni mtu mwenye akili timamu na anafanya maamuzi yake vizuri na kama wangeona hayuko sawa wangemshauri kwamba sio jambo jema lakini kuhusu swala la baba yao kufunga ndoa kwa kuoa mwanamke familia imelibariki kwani ni mzee na anahitaji uangalizi wa karibu zaidi.
Post A Comment: