Mbunge wa Jimbo la Butiama, Mhe. Jumanne Sagini (MB) amabye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akikagua sehemu ya Mto Mara uliopo katika Daraja la Kirumi lilioathiriwa na madaliko ya Maji katika Kijiji cha Kirumi, Wilaya ya Butima leo ikiwa ni moja ya Ziara yake Mkoani Mara.


Mbunge wa Jimbo la Butiama, Mhe. Jumanne Sagini (MB) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kirumi na Kijiji cha Kisakwe leo kwenye mkutano na wananchi wa jimbo lake.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Butiama Mkaruka Hamis Kura akizungumza na wananchi wa jimbo la Butiama leo katika Mkutano na wananchi hao katika Kijiji cha Kirumi leo, Machi 20, 2022.

..................................................

Na Mwandishi wetu.

Mbunge wa Jimbo la Butiama (MB) Mhe. Jumanne Abdallah Sagini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amewataka wananchi wa jimbo lake la Butiama kuondoa hofu kuhusu Mto Mara uliokuwa unasadikika kuwa na sumu.

Akizungumza na Wananchi wa jimbo lake la Butiama amewaomba kuamini taarifa iliyotolewa na Kamati Maalumu ya Kitaifa iliyoundwa na Serikali kuchunguza mabadiliko ya Maji ndani ya Mto Mara iliyotoa taarifa kwamba chanzo cha mabadiliko katika mto huo ni shuguli za binadamu pamoja na nguvu za asili.

“Jambo hili Serikali imetuondolea hofu tuamini kwamba tuko salama, Nasisitiza hakuna serikali duniani inapanga kuua raia wake, tahadhari zote zilizotolewa ilikuwa ni kujiridhisha na tuhuma hizo. Mto Mara upo salama mnaweza kuendelea kutumia ” alisema.

Mbunge Sagini ameyasema hayo wakati wa mikutano na wananchi wa Kijiji cha Wegero, kijiji cha Buswahili, Kijiji cha Kirumi, Kijiji cha Kitasakwa na kijiji cha Kwisero vilivyopo katika Wilaya ya Butiama baada ya kutembelea sehemu za Mto huo zilizoathiriwa kwenye jimbo lake la Butiama ikiwa ni moja ya ziara yake Mkoani Mara.

Aidha amewauliza wananchi hao kama kuna madhara makubwa yaliyotokea kwa mifugo yao baada ya kutumia maji ya mto huo na kuwaeleza kuwa kama mto huo ulikuwa una sumu basi ni lazima mifugo ingedhurika.

Hata hivyo amewasisitiza wananchi wa jimbo la Butiama kuhakikisha wanashirikia katika Sensa ya Watu na Makazi ifikapo mwezi Agosti 2022.

"Sensa ni muhimu sana itasaidia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia kuleta Maendeleo ya nchi"

Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Butiama, Mkaruka Hamisi Kura alisema kwamba majibu yaliyotolewa na Kamati Maalumu ya Kitaifa iliyoundwa na Serikali yanaendana na kilichozungumzwa na mwananchi wa kijiji cha Wegero aliyesema kabla ya ripoti hiyo kutangazwa.

Mwananchi huyo wa Kijiji cha Wegero anayeitwa Juma Waitaro alisema kuwa chanzo cha mchafuko wa Maji ya Mto Mara ni mimea aina ya magugumaji kwenye Mto huo kukauka kutokana na ukame na kisha kurundikana kwa muda mrefu ndani ya maji na kuchanganyika na vinyesi vya Mifugo. Mvua ziliponyesha zilitibua mimea hiyo na kupelekea mchafuko wa maji ndani ya mto huo.

"Mto unakitu inaitwa 'Eminyohu lulu itende' na lenyewe watu wanachimba samaki wadogo wadogo wakati wanachimba yale maozo yanakuwepo zilichimbwa mahala pengi tuu, lakini sasa maji yalipokuja yalikusanya vile vinyesi vya mifugo yakaingia kwenye mto yakakutana na yale maozo ya majani"
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: