NA JOEL MADUKA, GEITA 


Mbunge wa Jimbo la Busanda Wilayani  Geita Eng.Tumaini Magesa amewaomba wananchi wa Jimbo lake  kuupuza habari za Uzushi zinazosambaa Kuwa amesema hawajamchagua Bali  Amepewa nafasi hiyo  Kama zawadi .



Mbunge Magesa ameyasema hayo Kwenye mkutano wa adhara alioufanya Kwenye Kijiji Cha Mawemeru kata ya Nyarugusu ikiwa Ni Muendelezo ya Ziara Jimboni kwake Kusikiliza na kutatua changamoto na kero mbali mbali zinazowakabili  wananchi wake.



"Kuna watu wanaeneza propaganda kuwa nimepewa ubunge Kama zawadi sio kweli nyie ndio mlinipigie kura puuzeni Taarifa ambazo hazina msaada kwenye Jimbo letu la Busanda"Eng Tumaini Magesa Mbunge wa Busanda.


Aidha Magesa Hakusita pia kuwahakikishia Kuwa wananchi wajiandae kwa Maendeleo kwani Anaenda kufanya vitu vilivyoshindikana na wengine waliopita Kwenye Jimbo Hilo na Kuwaomba wapuuze maneno ya uchonganishi wanayoenezwa na watu wasio wema na maendeleo Ya Jimbo Hilo.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: