Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) DR Ritta Kabati akiongea na wanawake wa mkoa wa Iringa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) DR Ritta Kabati akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake. Baadhi ya wanawake wa mkoa wa Iringa wakiwa kwenye maandano ya kusherekea siku ya wanawake duniani.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MBUNGE wa viti maalum mkoani
Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) DR Ritta Kabati alisema licha ya
wanawake kudai masuala ya Usawa wa kijinsia ni muhimu wakatambua kuwa usawa unaozungumzwa
ni nafasi katika vyombo vya maamuzi na si katika ngazi ya familia kulingana na
mila na desturi Zilizopo
Akizungumzia maadhimisho ya siku
ya mwananmke Duniani Dr kabati alisema baadhi ya wananwake wamekosa uelewa wa
kutosha kuhusu mkakati wa kufikia lengo la usawa wa kijinsia hali inayochochea
wanawake walio wengi kuwa chanzo chas kuvunjika kwa ndoa
Dr Kabati alisema kuwa wanawake
wanatakiwa kuendelea kutekeleza wajibu wao kama wanawake katika familia ikiwepo
kuwaheshimu na kuwashirikisha kwenye majukumu mbalimbali waume zao ili
kudumisha ndoa zao kwa kuwa wanaume ni kichwa cha familia.
Aliwataka wanawake kuacha tabia
ya ulimbukeni kutokana na kipato na nyazifa walizonazo katika jamii badala yake
wanatakiwa kuendelea kutimiza wajibu kwa wanaume zao kama ambavyo mila na
desturi zinavyosema.
Dr kabati alisema kuwa wanawake
wengi hawajitambui ndio maana ndoa nyingi kwa miaka ya hivi sasa zimekuwa
zikivunjika bila sasababu za msingi kutokana na wanawake kuto waheshimu wanaume
zao.
Alisema kuwa analaani tabia ya
wanawake ambao wamekuwa wanafanyia tabia za dharau wanaume zao ambao ndio
kichwa cha familia na ndio kimekuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya familia hivi
sasa duniani.
Dr Kabati alisema kuwa wanawake
wanatakiwa kuwatunzia siri wanaume zao hata kama wamewazidi madaraka na kipato
hapo ndio ndoa itadumu kwa amani kwa sababu mke unakuwa umeshuka kwa mume wako.
Alisema kuwa jambo la hamsini
kwa hamsini kwa ngazi ya familia haliwezekani kutokana na mira na destori za
kiafrika kwa kuwa wanawake kutolewa mahari na wanaolewa hali ambayo inaweka wazi kuwa mwanaume ndio
kiongozi mkuu wa familia hata kama kipato chake ni kidogo.
Dr Kabati alisema wanawake
wengi waliofanikiwa kwenye nafasi mbalimbali ni wale waliojishusha na kuwashirikisha
wanaume zao hata kama wanavipato vidogo,kuheshimia na kuthaminia hapo itasaidia
kuleta amnai kwenye ndoa.
Alimalizia kwa kusema kuwa
wanawake wanatakiwa kuhakikisha wanawalea watoto wao kwenye malezi yanayotakiwa
katika jamii ili kuwa na kizazi ambacho kitakuwa na maadili katika jamiii.
Post A Comment: