Na Dotto
Mwaibale,Singida
KUELEKEA Sikukuu ya Wanawake Duniani ambapo kilele chake ni kesho Machi 8, Mbunge wa Viti Maalum ( CCM) Mkoa wa Singida Mhe. Aysharose Mattembe ametembelea Shule ya Sekondari Unyahati Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Akizungumza katika ziara ya kutembelea shule hiyo ikiwa ni moja ya shughuli yake katika kuadhinisha sikukuu hiyo Mhe Mattembe alisema pamoja na mambo mengine ziara yake hiyo imelenga kuzungumza na wanafunzi wa kike wa shule hiyo ikiwa ni kuwatia moyo ambapo amewataka wasome kwa bidii.
"Nawaombeni someni kwa bidii ili mutimize ndoto za maisha yenu kwa kuiga mfano wa Rais wetu Mama Samia Suluhu ambaye alisoma kwa bidii na kuzingatia masomo huku akiwa mtiifu na hatimaye leo hii ni Rais wa kwanza Mwanamke katika katika ukanda wa Afrika Mashariki" alisema Mattembe.
Mattembe aliwaambia wanafunzi hao kuwa kama watoto wa kike wanawajibu wa kuutambua utu wao, kuthubutu, kujithamini na kujiamini kwamba wanaweza.
Mbunge Mattembe ametumia nafasi hiyo kugawa taulo za kike kwa wanafunzi hao ikiwa ni njia mojawapo ya kuwapa hamasa na kutoacha kwenda shule wakati wanapokuwa katika siku zao za hedhi.
Mattembe alisema kauli mbiu ya sherehe za maadhimisho ya mwaka huu ni Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu"
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe.Miraji Mtaturu , Afisa Maendeleo Wilaya ya Ikungi Bi.Haika Masawe pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Ikungi.
Post A Comment: