Na,Jusline Marco:Arusha
Naibu waziri wa kilimo Mhe.Anthony Mavunde katika ziara yake amesema ili kuweza kufikia malengo ya wizara yaliyowekwa katika uzalishaji wa mbegu bora ushirikiano wa pamoja unahitajika ambapo amesema bado maeneo makubwa ya uzalishaji wa mbegu yabahitajika tofauti na ilivyo sasa.
Mhe .Mavunde ameagiza wakala wa mbegu Tanzania (ASA) kushirikiana na wadau walio katika tasnia ya kilimo cha mboga mboga na matunda kufahamu masoko ya mazao hayo ili kuweza kuongeza uzalishaji wa mbegu bora na miche na kuweza kuyafikia masoko hayo kwa urahisi zaidi huku akiagiza kituo cha utafiti wa kilimo (TARI) kuhakikisha wanafanya utafiti wa mbegu bora za mazao ya viungo yenye soko kubqa nje ya nchi.
Aidha ameziagiza halmashauri za Wilaya ya Arumeru kutenga maeneo maalum kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu bora na miche bora ili kuweza kuyafikia malengo ambayo wamejiwekea Kwani sekta ya mboga mboga na matunda ina mchango mkubwa hivyo kqa kuzingatia hayo kutaleta tija na matokeo ambayo yamekusudiwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mbegu za Kilimo (ASA) Dkt.Sophia Kashenge amesema uzalishaji wa mbegu umepanda kutoka tani 520 kwa miaka 4 iliyopita na kufikia tani 3033 huku malengo katika msimu ujao ni kufikia uzalishaji wa tani 6000.
Dkt.Kashenge ameyasema hayo katika ziara ya Naibu waziri wa kilimo Mhe.Anthony Mavunde iliyofanyika katika shamba la mbegu Ngaramtoni na Tengeru Wilayani Arumeru ambapo ameeleza kuwa uzalishaji huo wa mbegu umeongezeka kutokana na msukumo na uwezeshwaji wa serikali.
Adhi amesema lengo lao ni kutumia maeneo waliyonayo vizuri kwa ajili ya uzalishaji mbegu huku akieleza changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi imesababisha uzalishaji kupungua kutokana na mvua zinazonyesha kubadilika mara kwa mara.
Vilevile amesema baada ya kupokea fedha kutoka serikali kuu mashamba hayo yalianza kutumiwa yote katika shughuli za uzalishaji mbegu pamoja na kufanya ununuzi wa trekta 7 ,kujenga ofisi na maghala katika mashamba hayo hali itakayoongeza uwezo wa kuzalisha ambapo kwa mwaka 2022 uzalishaji umeongezeka hadi kufikia tani 3033 kutoka tani 1449.
"Tumeweka msukumo mkubwa katika kujenga maghala ili kukidhi uhifadhi wa mbegu ambazo tunazizalisha kwa sasa pamoja na maeneo ya kuchakata mbengu ndiyo maana tumefufua mtambo uliokuwa ukitumika zamani ili kukidhi ongezeko la uzalishaji."alisena Dkt.Sophia
Sambamba na hayo ameeleza kuwa kati ya hekta 600 zinazofaa kwa matumizi ya kilimo ni hekta 500 ambapo katika msimu ulipita waliweza kulima hekta 440 na waliweza kuvuna zaidi ya tani 600 na kueleza kuwa katika uzalishaji wa mbegu wanahitaji maeneo makubwa ili kupata eneo la utengano kati ya mbegu na mbegu kwa lengo la kuzuia uchaushaji wa nyuki na kujifadhi rutuba katika udongo.
"Asa tunatumia asilimia 28 ya ardhi katika kilimo huku sekta binafsi ikitumia asilimia 24 ya ardhi kwasabu nao ni wadau muhimu katika uzalishaji wa mbengu na nilazima tuwape maeneo kwasababu wanakosa maeneo yenye kukidhi ubora katika uzalishaji wa mbegu."Alisisitiza
Aliongeza kuwa mahitaji ya mbegu borq nchini ni takribani tani laki 3 za na ili kukidhi uzalishaji unaotakiwa hivi sasa kwa wingi wa wakulima uliopo ,takribani hekta laki mbili na nusu zinahitajika kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu bora kwani kwa sasa sekta ya serikali na sekta binafsi kwa umoja wao wana jumla ya hekta elfu 30 ya ardhi ambazo kwa wingi huo hazikidhi mahitaki ya uzalishaji
Pamoja na hayo Dkt.Sophia ameeleza kuwa muamko wa wakulima katika uzalishaji wa mbegu umekuwa mkubwa kutokana na watu kulima kilimo biashara hali inayosababisha watu kuwa na matumizi ya mbegu bora ambapo amesema halmashauri,taasisi za serikali na wizara zinapaswa kuunganisha nguvu ya pamoja ili kuweza kupata maeneo ya uzalishaji wa mbegu.
Post A Comment: