Mashirika ishirini ya kiraia yanayotetea haki za wafugaji wa asili Tanzania wameiomba serikali na wananchi wilayani Ngorongoro kukaa kwa pamoja katika meza ya mazungumzo ili kumaliza mgogoro wa ardhi uliopo katika wilaya hiyo.


Akitoa tamko hilo kwa niaba ya mashirika hayo katika mkutano wa mashirika hayo ,mkurugenzi wa mtandao wa wafugaji Tanzania bw,Joseph Parsambei amesema kuwa wamekutana ili kufanya tathmini na kuelimishana juu ya mgogoro huo na namna ya kuutatua.

Amesema kuwa wao wakiwa kama mashirika ya kutetea haki za wafugaji wanaomba pande zote mbili kukaa kwa pamoja huku wakiomba mashirika hayo ya kiraia kuhusishwa ili waweze kutoa ushauri wao kwa kuwa nao ni sehemu ya jamii.
Amesema kuwa wanatambua umuhimu wa uhifadhi na wanatambua haki za wananchi hivyo haki isikiukwe katika kutafuta uhifdhi.

Aidha amesema wanaunga mkono juhudi za kumaliza mgogoro huo huku kwa eneo la loliondo Sale wanasisitiza kuwepo kwa matumizi sahihi ya ardhi kwani ndio suluhisho la mgogoro huo.

Parsambei ameomba kila upande uheshimu sheria za nchi haki za binadamu na utawala wa kisheria huku wakitaka wadau wote kujielekeza katika meza huru ya majadiliano ili kumaliza mgogoro bila kuchochea upande wowote.

Kwa upande wake msaidizi wa kisheria kutoka shirika linalotoa msaada wa kisheria bi Agnes Marmo amesema kuwa wanaomba hatua zote zinazochukuliwa na serikali katika eneo la Loliondo Sale zishirikishwe kwa jamii husika ili kufikia muafaka .

Mkurugenzi wa mtandao wa wafugaji Tanzania  Joseph  Parsambei akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha  juu ya mgogoro wa Ngorongoro ameiomba Serikali kukaa meza ya mazungumzo
Msaidizi wa kisheria kutoka Shirika linalotoa msaada wa kisheria Agnes Marmo akisoma tamko lao ambapo aneiomba serikali ishirikishe jamii husika ili kupata muafaka



Share To:

Post A Comment: