Waziri wa Madini ,Doto Biteko, akizungumza juu ya mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.



Kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya awamu ya sita, Sekta ya madini imeweka historia kwa kushuhudia mauzo ya moja kwa moja yenye thamani ya shilingi trilioni 8.3 kutokana na mauzo ya madini aina mbalimbali.

Ameyazungumza hayo Leo Machi 1O, 2022 jijini Dodoma Waziri wa Madini Dkt Doto Biteko mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea mafanikio ya Sekta hiyo ya madini kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia.

Dkt Biteko amesema mauzo hayo yanatokana na madini ya dhahabu, madini ya fedha, madini ya shaba, makaa ya mawe, madini ya kinywe, madini ya Vito na madini ya ujenzi na viwandani. 

"Kutokana na biashara ya madini haya Wizara yetu imekusanya shilingi bilioni 597.53 Kama maduhuli ya Serikali yaliyokusanywa kupitia Wizara" - Dkt Biteko

Ushiriki wa watanzania kwenye Shughuli za madini umekuwa kutoka asilimia 48 hadi asilimia 63 na hivyo kuongeza thamani ya huduma migodini kufikia thamani ya dola za Marekani 579.3 sawa na Trilioni 1.33 kutokana na huduma zilizotolewa migodini

Hata hivyo Dkt Biteko amesema kati ya leseni takribani sita zenge uwekezaji mkubwa na wa kati zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji miradi hiyo .

Miradi ambayo ipo tayari kuanza Shughuli za uzalishaji ni mradi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Singida, mgodi wa Jumbo Lindi na uchimbaji madini ya Kinywe (graphite)anbayo ipo katika hatua za ujenzi wa miundombinu.

"Juhudi mbalimbali zimefanyika katika awamu hii za kupunguza adha za tozo zisizokuwa na tija kwa wananchi na wawekezaji katika Sekta ya Madini" - Dkt Biteko.

Hata hivyo Dkt Buteko amesema kufuatia uwekezaji unaofanywa na wawekezaji wa nje na ndani ya nchi wenye manufaa kiuchumi na kijamii kwa nchi na watu wote kwa ujumla na wananchi wa maeneo hayo ya miradi hiyo na watanzania wote wajenge tabia ya kutowasumbua wawekezaji kwa namna yoyote ile ikiwepo kuacha tabia inayofanywa na watu wachache kwenye miradi mipya inayoanzishwa.
Share To:

Post A Comment: