Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Bw. Adolf H Ndunguru akiongozana na Kamishna wa Madini Dkt. A. Mwanga atembelea Kituo cha Jemolojia Tanzania kwa lengo la kujionea utoaji mafunzo ya uongezaji thamani madni, shughuli mbalimbali za uongezaji thamani na utoaji wa huduma za utambuzi wa madini ya vito kwa wadau.

 Katika ziara hiyo ya alitembelea madarasa na karakana za uongezaji thamani madini hayo na kukutana na wanafunzi na kuongea na watumishi.  

Pamoja na ziara hiyo, Katibu Mkuu amepata muda wa kuongea na watumishi wa Kituoni. Akiongea na watumishi hao aliwapongeza kwa juhudi zao katika kutoa mafunzo na huduma mbalimbali kwa wadau kama vile utambuzi wa madini ya vito, ukataji wa madini ,uchongaji wa miamba na utengenezaji wa bidhaa za usonara kama pete, hereni n.k. 

Katibu Mkuu aliutaka uongozi na watumishi wote kuongeza juhudi katika uhamasishaji wa shughuli za uongezaji thamani madini nchini na kuongeza ubunifu zaidi, pamoja na kuongeza udahili ili kupata watanzania wengi zaidi wenye ujuzi, kutekeleza adhima ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuongezea thamani madini ndani ya nchi na kufikia malengo ya Wizara ya kuchangia Asilimia 10 kwenye pato la Taifa ifikapo





Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: