em>

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akizungumza kwenye Uzinduzi wa Mfuko wa Faraja wa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Christopher Kadio ambaye pia ni Mlezi wa Mfuko wa Faraja akizindua Mfuko wa Faraja wa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo, katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Christopher Kadio pamoja na Mwenyekiti wa Mfuko wa Faraja,Emmanuel Kayuni ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wakionesha nakala ya Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Watumishi ambao pia ni Wanachama wa Mfuko huo leo.

Katibu Mkuu, Christopher Kadio akikabidhi nakala ya Katiba ya Mfuko wa Faraja kwa baadhi ya Watendaji na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Fungu 51 ambao pia ni wanachama wa Mfuko wa Faraja leo katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Muda wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

...................................................................

Na Mwandishi wa MoHA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio ambaye pia ni Mlezi wa Mfuko wa Faraja ameagiza uongozi wa mfuko wa faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuzingatia katiba na mwongozo wa mfuko huo kwenye ukusanyaji wa mapato, matumizi ya fedha za mfuko huo na huduma kwa wanachama wake.

Akizungumza na uongozi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amewaelekeza kuingiza mchango wa mwajiri kwenye bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2022/23 ili kuhudumua wanachama wa mfuko huo. Pia amewaagiza kufanya uchaguzi wa Uongozi wa kudumu wa mfuko ndani ya mwaka huu wa fedha.

"Mimi kama Mlezi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi nawasisitiza kuzingatia katiba na mwongozo wa Mfuko hii pamoja na kuingiza mchango wa nwajiri kwenye bajeti ya Wizara" amesema

Christopher Kadio alisema hayo leo kwenye uzinduzi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi uliofanyika katika ukumbu wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto, jijini Dodoma.

Aidha amewashauri watendaji na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kujiunga na Mfuko huo kwani faida zake ni nyingi na utawawezesha wafanyakazi kiuchumi na kuongeza tija kwenye majukumu yao.

Katibu Mkuu Christopher Kadio amesema kwamba Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kama sehemu ya bima ya dharura na kwamba utasaidia kupunguza msongo wa mawazo wa changamoto za masuala ya dharura ya kijamii kama kuuguliwa na kufiwa.

“Licha ya kwamba kujiunga na Mfuko ni hairi ya mtu,lakini kwa faida nilizozieleza ni ushauri wangu kuwa watu wote wajiunge kwa kuzingatia faida nilizozieleza, Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu” alisema.

Share To:

Post A Comment: