Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine (kulia chini) akizungumza kutoka Shinyanga Tanzania na Wazeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa (Sibongile Tsoanyane (kushoto) na Sussie Mjwara (kulia juu) wakishiriki mafunzo hayo wakiwa Afrika Kusini. Kushoto ni Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakiwa katika ukumbi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga wakishiriki mafunzo hayo kwa njia ya Mtandao (Tele Conference).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika lisilo la kiserikali la Investing in Children and Strengtherning their Societies (ICS ) linalohusika na masuala mbalimbali ikiwemo malezi na makuzi bora ya watoto,ulinzi na usalama kwa watoto na wanawake limetoa mafunzo kwa wafanyakazi wake 22 kuwajengea uwezo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Programu Tumishi (Aplikesheni) ya Parent App.

 

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo ya siku nne yaliyoanza leo Jumatatu Machi 28,2022 katika ukumbi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga, Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine  amesema timu ya ICS inajifunza na kujinoa kila siku kuendana na kasi ya kukua kwa teknolojia duniani.

 

Amesema mafunzo hayo yanafanyika kwa njia ya mtandao (Tele conference) na shirika la Crown Without Borders South Africa na wafanyakazi wa ICS Tanzania wapatao 22 wanajengewa uwezo kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi mpya wa Parenting for Life Long Health (PLH).


“Mafunzo kwa wafanyakazi 22 wa Shirika la ICS kwa ajili ya kujifunza mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App  ni sehemu ya kujijengea uwezo kabla ya kuanza utekelezaji yanafanyika kwa njia ya mtandao (Tele conference) na shirika la Crown Without Borders South Africa.  Baada ya mafunzo haya kazi ya utekelezaji itaanza katika mkoa wa Mwanza na Shinyanga ”,amesema Kudely.

 

“Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kidunia wa kufikisha elimu ya malezi na makuzi bora ya mtoto ili kuondoa ukatili  dhidi ya watoto na wanawake (The Global Parenting Initiative) . Sisi ICS tumeanza mafunzo haya ili kutekeleza mkakati huu kupitia mradi wa Parenting For Life Long Health (PLH) ambapo tunashirikiana na taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika Kusini”,ameeleza Kudely.


Amefafanua kuwa Shirika la ICS litakuwa linafanya utekelezaji wa mradi huo kwa kushirikiana na taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika Kusini na kufanya utafiti wa kina ili kutambua ni kwa kiasi gani kufikisha elimu ya malezi na makuzi bora ya mtoto kwa njia ya kidigitali na inaleta tija ili kupunguza ukatili dhidi ya watoto na wanawake.


“Tunaanza utekelezaji wa  mradi huu mkoani Shinyanga na Mwanza na awamu ya kwanza tumepanga kufikia wazazi/walezi 1100 na awamu ya pili tunatarajia kutanua utekekezaji na kufikia mikoa Zaidi ya 6 Tanzania na kufikia wazazi /walezi wasiopungua 6000”,amesema Kudely.


Ameongeza kuwa Utekelezaji wa mpango huu umekuja kama sehemu ya ubunifu (Innovation) wa namna ya kufikisha elimu katika jamii kwa njia ya teknolojia na kuwafikia wanufaika wengi zaidi ili kuleta mabadiliko na kuchangia kuondoa ukatili dhidi ya watoto na wanawake. 

“Na sisi kama ICS kila wakati tunapotekeleza afua zetu tunajifunza na kuja na ubunifu ambao unaweza kuleta tija Zaidi katika jamii lakini pia kufanya tafiti zitakozopima na kuthibitisha afua tunazotekeleza zinaleta matokeo chanya (Evidence Based Intervention)”,amesema

 

“Sisi kama ICS na washirika wetu (Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika Kusini) tunajitahidi kila siku kuwa wabunifu na kuja na mikakati ambayo inaweza kutumia rasilimali kidogo na kuleta matokeo makubwa katika afua zetu zote tunazozitekeleza”,ameeleza. 

Amefafanua kuwa Utekelezaji wa mradi huu (Pareting for Life Long Health-PLH) wa kutoa elimu ya malezi na makuzi ya bora ya mtoto kwa njia ya kijitali utachangia mpango wa dunia (The Global Parenting Initiative-GPI) wa kufikisha elimu ya malezi wa wazazi/malezi na pia mpango wa Taifa (NPA-VAWC) wa kupunguza Ukatili dhidi ya watoto wa wanawake na watoto.

“Wazazi/Walezi wengi wana simu kwa hiyo tumebuni namna ya kuwafikishia elimu kwa njia rahisi kabisa na inayotumia muda mfupi maana ParentApp mzazi/mlezi anaweza kuitumia hata wakati hayupo kwenyeInternet akajifunza na kupata ujumbe murua kabisa kuhusu malezi na makuzi bora ya watoto”,amesema Kudely.

Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine akizungumza leo Jumatatu Machi 28,2022 wakati wa mafunzo kwa wafanyakazi 22  wa Shirika la ICS kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Programu Tumishi (Aplikesheni) ya Parent App. Mafunzo hayo yamefanyika kwa njia ya Mtandao (Tele Conference). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakimsikiliza Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa Sussie Mjwara (kulia) akielezea kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS (kushoto) wakimsikiliza Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa Sussie Mjwara (chini) akielezea kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS  (kushoto juu) wakimsikiliza Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Sibongile Tsoanyane (chini) akielezea kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakifuatilia mafunzo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine akifuatilia mafunzo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakifuatilia mafunzo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakifuatilia mafunzo kuhusu mkakati wa namna ya kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting) kupitia Parent App.Wa kwanza kushoto ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Alex Nyembele.
Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Stivin Mwakakeke akielekeza wafanyakazi wa ICS  namna kutumia  Parent App ambayo inasaidia katika kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting).
Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Stivin Mwakakeke akiwaelekeza wafanyakazi wa ICS  namna kutumia  Parent App ambayo inasaidia katika kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting).
Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Stivin Mwakakeke akiwaelekeza wafanyakazi wa ICS  namna kutumia  Parent App ambayo inasaidia katika kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya watoto kwa njia ya kidigitali (Digital Parenting). Wa kwanza kushoto ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka shirika la Crown Without Borders South Africa, Alex Nyembele.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakipiga picha ya kumbukumbu.
Wafanyakazi wa Shirika la ICS wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share To:

Post A Comment: