Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt Joyce Nyoni akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii,Kijitonyama Dar es salaam.

Mwenyekiti wa chama cha wataalamu wa ustawi wa jamii Dkt. Mariana Makuu akitoa ufafanuzi juu ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani katika mkutano na vyombo vya Habari,kijitonyama Dar es salaam.

Wadau wa Ustawi wa Jamii na Waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama,Dar es salaam.

Wadau wa Ustawi wa Jamii kutoka Taasisi ya Ustawi wa Jamii,TWASO na TaCosWe wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mkutano na vyombo vya Habari.

*************************

Katika kuadhimisha kilele cha siku ya Ustawi wa Jamii Duniani yenye kauli mbiu “Juhudi jumuishi dhidi ya ukatili wa aina zote kwa maendeleo endelevu” Taasisi ya Ustawi wa Jamii ikishirikiana na Chama cha watoa huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) na Umoja wa mashirika yasiyo yakiserikali ya ulinzi na huduma za Ustawi wa Jamii (TaCosWe) na wadau wengine watatoa huduma za Ustawi wa Jamii bure kwa wananchi wote siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani tarehe 15/03/2022 na kuendelea.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt Joyce Nyoni,amesema ni Mwaka wa kuminatano sasa tunaadhimisha siku ya Ustawi Duniani kote tangu ilipoanza kuadhimishwa mwaka 2007.

Alisema ili kuiishi kauli mbiu ya mwaka huu Taasisi na Wadau tutatoa huduma ushauri wa masuala ya Ndoa na mahusiano, masuala ya watoto waliotelekezwa na ushauri wa kisaikolojia na nyingine nyingi pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu hasa nini Maana ya Ustawi wa Jamii na wawatumue vipi wataalam hawa kutatua changamoto za kila siku kwenye maisha.

"Nawakaribisha wananchi wote kupata huduma za jamii na elimu zitakazo tolewa bure katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii"

Naye mwenyekiti wa chama cha wataalamu wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) Dkt Mariana Makuu amesema “Sababu kubwa ya ukatili unaoendelea hapa nchini ni Afya ya akili, tunawakaribisha wananchi wote waje waongee na wataalamu ambao watawasaidia kutatua matatizo yao” Kwa Upande wake Katibu wa umoja wa mashirika yasio ya kiserikali ya ulinzi na huduma za jamii Bi Hilda Ngaja amesema "Tunashirikiana na Serikali na Wadau wengine katika kustawisha Jamii yetu na kuondoa tatizo hili la ukatili linalo endelea nchini kwetu"
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: