Charles James
MWAKA mmoja! Mwaka mmoja wa Utumishi uliotukuka, uzalendo, upendo na utu. Mwaka mmoja wa ushujaa kwake na kwa watanzania. Mwaka mmoja wa historia.
Tutarudi hapa kwenye mwaka mmoja siku nyingine, Tuendelee.
Duniani kote leo ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake, nami katika bandiko hili nimechagua kuadhimisha Siku hii na Mwanamke shupavu, jasiri, mvumilivu na mwenye upendo kwa watanzania kuliko hata ilivyo kwa familia yake.
Ni wengi wanaweza kuwa Wanawake Majabali katika Taifa letu, lakini huyu naemzungumzia leo katika Siku hii ya Wanawake ni Mwanamke ambaye Mwenyezi Mungu amemuinua katikati ya Wanawake wenzie na Wanaume wa Taifa hili.
Mwanamke ambaye baada ya Taifa kuingia Kwenye jaribio la kumpoteza Rais wa Nchi (Hayati Dk John Magufuli) macho yetu yakatua kwake ili aweze kutuvusha kama Rais wetu.
Tanzania haikuwahi kumpoteza Rais akiwa madarakani, lakini Mwaka jana (2021) ilitokea kwa mara ya kwanza.
Katiba ikamtaka Makamu wa Rais achukue Nchi, naye akaapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wafitini na wenye chuki wakadhani hatoweza, Tazama vichwa vyao viko chini kwa namna alivyofanya kazi kubwa ya kuijenga Tanzania yetu Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa na Kimataifa.
Happy Women Day, Rais Samia Suluhu Hassan, Heri ya Siku ya Wanawake Shujaa wetu na kiongozi wetu.
Mwenyezi Mungu alikuinua ukawa Makamu Mwenyekiti katika Bunge lile gumu la Katiba lakini ukafanikiwa kuwa kipenzi cha kila mjumbe.
Allah akakuinua tena mwaka 2015 ukawa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke, ukafanya kila mtanzania avutiwe na wewe. Kila mtanzania amuite mtoto wake wa kike Samia.
Wakati tukidhani imetosha, jina lako linachorwa tena na Mwenyezi Mungu kuwa Rais wa Kwanza Mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bado umeweka rekodi nyingine kubwa ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza Mwanamke wa Chama Cha Mapinduzi CCM (Taifa), tuseme nini juu yako wewe Mwanamke mwenye upendo na ngozi ya uongozi?
Nina mengi ya kusema kwenye mwaka mmoja wako wa Urais Mama lakini wacha niyahifadhi kwa ajili ya kilele chenyewe cha mwaka mmoja.
Leo nikutakie Siku Njema ya Wanawake huku nikikuomba utambue kwamba kupitia wewe Wanaume wengi wamebadilisha mitazamo yao kuhusu watoto wa kike, kupitia wewe Tanzania itazalisha Wanawake wengi majabali na wenye wivu wa maendeleo.
Kupitia wewe ipo siku atazaliwa Samia mwingine katika Taifa hili hili lililomzaa Bibi Titi Mohamed, Amina Salum, Asha Rose Migiro, Maria Nyerere, Fatma Karume na wengineo wengi.
Wewe ni kielelezo cha "Wanawake Wanaweza" Enjoy your day Mom!😍 #kaziiendelee
Post A Comment: