Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Paulne Gekul Machi 21. 2022 Jijini Dodoma amewapongeza wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kwa kuchaguliwa na kuaminiwa kuwa wanaweza kusimama mbele na kuwawakilisha wenzao katika mkutano huu wakitoka katika idara na vitengo vyao.
Naibu Waziri Gekul aliongeza kuwa yeye jukumu lake ni kumsaidia Waziri Mchengerwa kwa kuyafanikisha malengo ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na taifa letu linasonga mbele.
Post A Comment: