Adeladius Makwega-WUSM.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbasi ambaye ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wizarani hapa Machi 21, 2022 amefungua  mkutano wa baraza hilo unaofanyika kwa siku mbili unaohudhuria na wajumbe kadhaa huku akiwapongeza wajumbe wapya kwa kuchaguliwa tena katika nafasi hizo.


“Unapochanguliwa tena maana yake umeaminiwa na wenzako kuja kuwawakilisha tena na hata kama wewe ni mjumbe mpya maana yake umeaminiwa kuja kuwawakilisha kwa nafasi hiyo, nawapongeza sana.”


Mara baada ya ufunguzi huo, ulifanyika uchaguzi wa Katibu wa Baraza hilo ambapo Bernard Lubogo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Sera na Mipango alimshinda Bi Sofia Limbu Afisa Utamaduni Mwandamizi kwa kura 35 kwa 2.


Mwanzoni mwa kikao hicho Katibu Mkuu Dkt Abbasi alimtambulisha Naibu Katibu Mkuu Said Othumani Yakub kwa kuwa hiki ni kikao chake cha kwanza tangu ateuliwe.


Baraza la Wafanyakazi ni chombo cha kisheria kazini ambacho kinatoa nafasi kwa watumishi wa taasisi kuyajadili mambo kadhaa ya taasisi yanayotoka kwa viongozi na yale yanayotoka kwa wafanyakazi.


Share To:

Post A Comment: