Na HERI SHABAN
DIWANI wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Beatrice Edward amewataka Wanawake kujikwamua kiuchumi kwa kufanya kazi za kujishughulisha na kubuni miradi ya Maendeleo.
Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Beatrice Edward alisema hayo katika madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kata ya Kitunda,Mzinga na Kivule .yalioandaliwa na Taasisi zinazoshughulika kuisaidia Wanawake Green Kinds and Youth fondation Kwa kushirikiana na Open Mind and thoughts Organization.
"Nawaomba Wanawake wezangu tujikwamue kiuchumi Ili tujikomboe kimaisha tuwe wabunifu katika kubuni miradi ya Maendeleo itakayotuwezesha kupata kipato "alisema Beatrice.
Aliwataka watumie fursa zao vizuri katika kusaka masoko ya Biashara ndani na nje ikiwemo kujenga mtandao wa biashara utakaowawezesha kuuza biashara zao katika masoko makubwa ..
Aidha aliwataka watumie fursa zao katika medani ya Siasa katika kugombea nyasifa mbalimbali za uongozi kwani Wanawake wanaweza.
Aliwataka Wanawake Wilaya ya Ilala kusonga mbele katika ujasiriamali na kutafuta masoko Kimataifa .
"Wanawake wezangu mnaweza Leo ni siku yetu muhimu nawaomba tujikwamue kiuchumi na kuunga mkono juhudi za Rais wetu wa TANZANIA Samia Suluhu Hassan katika kukuza uchumi viwanda Tanzania Rais wetu ametimiza mwaka mmoja ameupiga mwingi Wanawake tunajivunia alisema.
Akiwataka Wanawake wakope mikopo ya Halmashauri na kurejesha kwa wakati Ili wengine waweze kukopa mikopo hiyo
Wakati huo huo Diwani Beatrice Edward aliwataka Wanawake kushiriki SENSA ya makazi Kwa ajili ya KUHESABIWA kwa ajili ya Maendeleo ya nchi na Taifa kwa ujumla
Rais wa Vikoba vya Wanawake Tanzania Devota Likokora aliwataka Wanawake Wilaya ya Ilala na Ukonga wamtumie Selemani Bishagazi vizuri kwa ajili ya Maendeleo ya Wanawake na uchumi kwa ujumla
Devota Likokora aliwataka Wanawake Jimbo la Ukonga kumtumia vizuri Mkurugenzi wa Sauti ya Jamii Kipunguni Selemani Bishagazi katika katika kusaidia Wanawake kupitia Taasisi ya SAUTI ya Jamiii.
Devota Likokora aliwataka Wanawake kuwatumia vizuri Maafisa Maendeleo wa Ukonga Kwa ajili ya Maendeleo ya Wanawake pamoja na Jamii kwa ujumla.
Aliwataka Wanawake kukopa mikopo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo inatolewa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hasan ambayo aina riba yoyote.
Post A Comment: