Na,Jusline Marco:Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ametoa muda wa siku 30 kwa halmashauri ya Wilaya ya Meru kuhakikisha wanafuta vibali vya viwanja vilivyotolewa kinyemela katika eneo la hifadhi ya mto Usa.
Akizungumza kwenye zoezi la upandaji miti lililofanyika katika mto huo Wilayani Arumeru, Mhandisi Ruyango pia ameagiza kutolewa katazo kwa wakulima wanaolima mazao yao pembezoni mwa mto huo kuyaondoa ili kuacha eneo la mto huo kuwa salama.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Jeremia Kishili amesema kuwa maji ni uhai na maji hayana mbadala hivyo,amesema halmashauri hiyo itahakikisha inasimamia vyanzo vyote vya maji vinahifadhiwa.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Nkoanekoli ,Braham Nanyaro amesema zoezi la uoteshaji wa miti litaboresha upatikanaji wa maji na utunzaji wa mazingira.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani,Muaidolojia Philipo Patrick amesema eneo ambalo wamelichagua kuotesha miti linachangamoto za uhifadhi ambapo amesema mita 60 za kuhifadhi vyanzo vya maji na mito zipo kisheria na hazipaswa kuingiliwa kwa shughuli zozote zile.
Muaidolojia kutoka katika Bodi ya maji Bonde la Pangani,Philipo Patrick akizungumza kwenye zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Mto Usa ikiwa ni moja ya uadhimishaji wa wiki ya maji.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nkoanekoli ,Braham Nanyaro akipanda miti katika eneo la akiba la Mto Usa kwa niaba ya wakijiji wake lengo ni kuhamasisha utunzaji wa vyanzo vya maji.
Kibao kilichowekwa na Bodi ya Maji Bonde la Pangani kikiwa na ilani ya katazo la ufanyaji wa shughuli za kibinadamu katika mto Usa.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nkoanekoli walioshiriki zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Mto Usa kwenye Wiki ya Maji.
Post A Comment: