Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na baadhi ya wananachi wa wilaya ya Iringa kuhusu jukumu la kutunza vyanzo vya maji.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na baadhi ya wananachi wa wilaya ya Iringa kuhusu jukumu la kutunza vyanzo vya maji.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na baadhi ya wananachi wa wilaya ya Iringa kuhusu jukumu la kutunza vyanzo vya maji.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na baadhi ya wananachi wa wilaya ya Iringa kuhusu jukumu la kutunza vyanzo vya maji.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo kuwachukulia hatua Kali za kisheria
wananchi na viongozi wote watakao hatibu vyanzo vya Maji na kukata hovyo miti.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya maji wilaya ya
Iringa yaliyofanyika katika Kijiji Cha magunga alipokuwa akishilikiana kupanda
zaidi ya miti Mia tano ambayo ni rafiki ya maji.
Moyo alisema Kuwa Serikali imekuwa inatumia gharama kubwa kuhifadhi
vyanzo vya maji na kuwapelekea maji Wananchi Lakini Wananchi wamekuwa
wakiharibu vyanzo vya maji kwa makusudi bila kujali Serikali imetumia gharama
kiasi gani.
Alisema kuwa maadhimisho ya wiki ya maji ya mwaka huu 2022
ambayo yameanza rasmi tarehe 16/03/2022 na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe
22/03/2022 lengo kubwa ni kukumbushakutunza rasmali za maji ni maisha ya
wanadamu wote.
Moyo alisema kuwa wilaya
ya Iringa inaendelea kutoa huduma ya maji safi na salama kwa maeneo yote ya
vijijini kwa wastani wa asilimia 75.6 na Iringa mjini imefikia asilimia 97 na
hayo yote yanaendelea kuboreshwa zaidi na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Samia Suruhu Hassan.
Alisema kuwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suruhu Hassan anatambua adha ambayo wananchi wanaipata hasa wanawake kwenda
kufuata maji umbali mrefu na kusababisha kero nyingi kwenye familia.
Moyo alisema katika mwaka wa fedha wa 2021/2122 wilaya ya Iringa
inaendelea kukarabati miradi mbalimbali ya maji ikiwepo ya vijiji vya Nyabula/Ulanda,Magunga/Itengulinyi,Makatapola,Mbweleli,na
Makuka yote kwa lengo la kuhakikisha wanawatua ndoa wakinamama wa wilaya hiyo.
Alisema kuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suruhu Hassan amefanikiwa kupata fedha na kuanza kutekeleza miradi mingine
zaidi kupitia Mpango wa Maendeleo ya ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya
Uviko -19 ambayo imeanza kutekelezwa katika majimbo ya Kalenga na Isimani.
Moyo alisema kuwa katika wilaya ya Iringa wamejipanga kikamilifu
kuhakikisha kuwa wanaendelea kuvilinda vyanzo vya maji na kupanda mti ambayo
inasaidia kutunza maji yaliyopo ardhini kwa ajili ya matumizi.
Alisema kuwa wataendelea kuitumia kauli mbiu ya maazimisho ya
maji mwaka huu inayosema kuwa “maji chini ya ardhi,hazina isiyoonekana kwa
maendeleo endelevu” kwa kvitunza vyanzo vyote ya maji vilivyopo wilaya ya
Iringa.
Kwa upande wake meneja wa RUWASA wilaya ya Iringa Eng Masoud
Samila alisema kuwa katika maadhimisho ya siku ya maji wilaya ya Iringa
yaliyofanyika katika Kijiji Cha magunga wamefanikiwa kupanda jumla ya miti mia
tano (500) ambayo ni rafiki na maji.
Eng Samila alisema kuwa lengo la serikali kuhakikisha inamtua
ndoo mama kichwani na kuwasaidia wananchi wa wilaya ya Iringa kupata maji safi
na salama kwa ukaribu ambao utasaidia kuendelea kufanya shughuli nyingine za
kimaendeleo.
Post A Comment: