Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akizungumza katika eneo panapojengwa mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji kwenye Mradi ya maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji, kutunza miundombinu ya maji pamoja na kutumia maji safi na salama kwani serikali imetumia gharama kubwa kuwafikishia huduma ya maji.
Mkude ameyasema hay oleo Jumanne Machi 22,2022 wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
“Tunapoadhimisha wiki ya maji ni vyema tukakumbushana sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia masuala ya maji kama vile kutofanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika chanzo cha maji,kutokuharibu mazingira kwa kukata miti hovyo na kuchoma moto misitu,kutunza miundo mbinu ya maji tukitambua kuwa serikali inatumia gharama kubwa kufikisha huduma ya maji kwa wananchi”,amesema Mkude.
“Kauli mbiu ya Wiki ya Maji mwaka huu ni ‘Maji chini ya ardhi hazina isiyoonekana kwa maendeleo endelevu’,hii ina maana kubwa sana kwamba kutunza,kuhifadhi na kulinda vyanzo vya maji yakiwemo yanayopatikana chini ya ardhi, kutunza uoto wa asili na kupanda miti rafiki na vyanzo vya maji”, ameeleza Mkude.
Mkuu huyo wa wilaya amesema Serikali inaendelea na jitihada za kufikisha maji katika maeneo ya vijijini ambako kuna asilimia 80 ya wakazi kwa kufanya tafiti ya vyanzo vya maji na kujenga miundombinu hivyo kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa maji wanapofika kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na kulinda vifaa na rasilimali zinazoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.
“Serikali inaendelea na jitihada kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inapatikana Mijini na Vijijini ambapo RUWASA Kishapu kwa sasa inawafikia wananchi kwa asilimia 56.5 kutoka 42.3% mwaka 2015”,amesema Mkude.
Mkude ametumia fursa hiyo kuipongeza RUWASA kwa kuendelea kutekeleza vizuri miradi ya maji huku akiwataka Wakandarasi kuongeza kasi ya kutekeleza miradi ya maji inayoendelea kujengwa ukiwemo wa kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba, Miradi ya maji Bubiki Bupigi – Butungwa.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu , John Lugembe amesema wanatekeleza ujenzi wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ikiwemo kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba, Miradi ya maji Bubiki Bupigi – Butungwa, Miradi ya maji Igaga – Isagala hadi Lagana na michakato inaendelea kwa ofisi ya RUWASA kuainisha maeneo mengi zaidi ili kufikia lengo la wananchi vijijini kupata maji safi na salama.
Amesema lengo la miradi hiyo ya maji ni kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi ili kuboresha hali ya maisha na kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na kumtua mama ndoo kichwani kwa kumpunguzia umbali wa kwenda kutafuta mmaji na badala yake kumuongezea muda wa kufanya shughuli zingine za maendeleo ili kujiimarisha kiuchumi na kijamii.
Akitoa taarifa ya hali ya huduma ya maji vijijini na utekelezaji wa miradi ya maji, Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Winfrida Emmanuel amesema katika kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Kishapu wanapata huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza katika maeneo ya vijijini na Miji Midogo ya wilaya, wamejikita katika ukarabati wa visima na miradi ya maji yenye kuleta matokeo ya haraka kuongeza upatikanaji wa maji.
“Ujenzi/upanuzi/ukarabati/uboreshaji wa miradi ya maji kwa sasa unatekelezwa kupitia fedha za Programu ya PV4, PbR, NWF na UVIKO – 19 ambapo utekelezaji wake unafanywa na Wakandarasi wajenzi na Watalaamu wa RUWASA”,amesema Emmanuel.
Amesema katika wilaya ya Kishapu kuna jumla ya miradi ya maji ya bomba 19, bwawa moja, visima vifupi 158, visima virefu 13 na matenki ya kuvuna maji ya mvua 173 iliyokwisha kamilika na inahudumia vijijin 69 kati ya vijiji 125 vilivyopo katika wilaya ya Kishapu inayokadiriwa kuwa na wakazi 350,503 (Projection 2021).
Diwani wa kata ya Bubiki Mhe. James Kasomi pamoja na wakazi wa Bubiki wameishukuru serikali kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwani hapo awali walikuwa wanatumia muda mwingi kufuata huduma ya maji kwenye mabwawa.
Kabla ya kuzungumza na wakazi wa kata ya Bubiki katika mkutano wa hadhara, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude ametembelea na kukagua ujenzi wa Miradi ya maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa na kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba na kujionea kazi ya kufyatua tofali,kujenga minara ya matanki na matanki ya kuhifadhia maji ikiendelea chini ya usimamizi wa RUWASA.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akikagua ubora wa matofali leo Jumanne Machi 22,2022 kwenye Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa ambapo kazi ya kufyatua tofali,kujenga mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji inaendelea kutekelezwa na Mkandarasi Bent Company Limited chini ya usimamizi wa RUWASA wilaya ya Kishapu. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu , John Lugembe ( wa pili kulia) akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude kuhusu ujenzi wa Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa kata ya Bupigi wilayani Kishapu.
Fundi akitoa tofali ndani ya maji baada ya kuwekwa siku 7 kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa kata ya Bupigi wilayani Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akizungumza katika eneo panapojengwa mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji kwenye Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akizungumza katika eneo panapojengwa mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji kwenye Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Bupigi – Butungwa.
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu , John Lugembe ( kushoto) akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) kuhusu ujenzi wa Mradi wa maji ya bomba wa kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba ambapo kazi ya kufyatua tofali,kujenga mnara wa tanki na tanki ya kuhifadhia maji unaendelea chini ya usimamizi wa RUWASA.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (katikati) akizungumza katika eneo ambapo matofali kwa ajili ya Mradi wa maji ya bomba wa kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba yanafyatuliwa.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto mwenye suti ya bluu) akizungumza katika eneo ambapo ujenzi wa mnara wa tanki na tanki la kuhifadhia maji kwenye Mradi wa maji ya bomba wa kata ya Bubiki katika vijiji vya Mwamishoni na Nyasamba unaendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) akifungua bomba la maji katika moja ya magati ya mradi wa maji uliopo katika kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) akimtua kichwani ndoo ya maji mmoja wa wanawake katika kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) akimtua kichwani ndoo ya maji mmoja wa wanawake katika kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika leo Jumanne Machi 22,2022 katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Wakazi wa Bubiki wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Mhe. Shadrack Kengese akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA wilaya ya Kishapu, Neema Mwaifuge akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Winfrida Emmanuel akisoma taarifa ya hali ya huduma ya maji vijijini na utekelezaji wa miradi ya maji kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA wilaya ya Kishapu, Neema Mwaifuge
Diwani wa kata ya Bubiki Mhe. James Kasomi akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Mwenyekiti wa kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki Mhe. William Singu akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Akina mama wakazi wa Bubiki wakiishukuru serikali kwa kuwaletea huduma ya maji safi na salama kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo katika Wilaya ya Kishapu yamefanyika katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki.
Wananchi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Wananchi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Wafanyakazi wa RUWASA wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Wafanyakazi wa RUWASA Kishapu na viongozi mbalimbali wa Bubiki wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Wananchi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji katika Kijiji cha Bubiki kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Post A Comment: