Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo akihutubia. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Taifa ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Shani Ulumbi, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Monica Samwel, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Iramba, Rydia Kidaila na Katibu wa UWT, Catherine Sarwat.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Taifa ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Shani Ulumbi akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Sherehe zikiendelea. |
Na Dotto Mwaibale,
Iramba
MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda ameiomba
Serikali kuandika upya historia ya wapigania Uhuru nchini ili kutoa fursa ya
kuigizwa kwa wapigania Uhuru wanawake
ambao nao walifanyakazi kubwa ya kupigania uhuru lakini kwenye historia hawakujumuishwa.
Mwenda
alitoa ombi hilo jana katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo
yalifanyika Kiwilaya katika Kijiji cha Kyalosangi wilayani humo na kusisitiza kuwa kuandikwa
kwa historia upya ya wapigania Uhuru itasaidia kwa kiasi ki kubwa vizazi vya sasa
na vijavyo kujua jinsi wanawake walivyo shiriki kikamilifu katika kutafuta uhuru wa
Tanzania.
Akimtolea
mfano wa mmoja wa mwasisi Mwanamke aliyejitoa kwa hali na mali katika kupigania
Uhuru wa Tanzania Khadija Kamba ambaye hajawahi kuandikwa sehemu yoyote kwenye
historia ya wapigania Uhuru Mwenda alisema waasisi hawa historia yao inapaswa
kuandikwa kwa faida ya Taifa letu.
Alimtaja
mwasisi mwingine kuwa ni Mke wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,
Mama Maria Nyerere ambaye wakati mume wake alipoacha kazi ya kufundisha na
kuanza harakati za kupigania uhuru yeye alifungua duka maeneo ya Kariakoo
ambapo alikuwa akiuza mafuta ya taa na kupata fedha za kuendeshea maisha yao.
“Mama
Nyerere kwa namna moja hama nyingine anaingia katika historia hiyo licha ya
kwamba naye hajaandikwa mahali popote katika ushiriki wake wa kupigania nchi
hii” alisema Mwenda.
Akizungumzia
kuhusu vitendo vya ukatili kwa wanawake alisema katika wilaya hiyo bado kuna baadhi
ya jamii zinaendelea kukumbatia mila potofu ikiwemo ya kuwanyima mirathi wanawake
wajane jambo ambalo linatakiwa kukomeshwa katika jamii.
“Sisi kama Serikali katika ngazi ya wilaya
tumeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha tunaziondoa mila zote potofu
na kandamiz” alisema Mwenda.
Aidha Mwenda alisema wilaya hiyo
imekomesha vitendo vya
ukeketaji wawanawake na wasicha kutokana na kuimarishwa kwa utoaji wa elimu kuhusu
madhara ya ukeketaji katika jamii.
Alisema kazi
iliyofanyika na kukomesha vitendo hivyo wilayani humo ni kubwa ambapo ameitaka jamii
kutorudi nyuma na kurudia vitendo hivyo ambayo vinadhalilisha utu wa mtu.
Katika hatua
nyingine alisema Halmashauri hiyo kupitia mikopo inayotolewa kutoa asilimia 10
ya mapato ya ndani kwa mwaka 2020/2021 jumla ya Sh.59,758,624.39 ilitolewa
katika vikundi tisa vya wanawake ambapo pia kwa mwaka 2021/2022 jumla ya
Sh.17,301,745.70 zilitolewa katika vikundi vitatu vya wanawake na kuwa jumla ya
vikundi 12 vilivyopata mkopo wenye jumla ya Sh.77,060,370.09.
“Leo hii
tunapoadhimisha maadhimisho haya Halmashauri inatoa mikopo kwa vikundi viwili
vya wanawake ambavyo ni Kikundi cha
Tumaini kilichopo Kijiji cha Tyeme Kata ya Mtoa ambacho kinapewa mkopo wa
Sh.20,000,000 na kikundi cha Nansule kilichopo Kijiji cha Ntwike ambacho
kinapewa Sh.7,520,000 na kufanya jumla ya vikundi vyote vya wanawake
vilivyopewa mkopo kuanzia mwaka 2020/2021 hadi mwaka 2021/ 2022 kufikia vikundi
14 vilivyopewa mkopo wenye thamani ya jumla ya Sh.104,060,370.9.
Akisoma risala ya maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo “Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendfeleo Endelevu” Msoma Sara Mitula alisema jamii inapaswa kutambua kuwa maendeleo endelevu ni lazima yahusishe jinsia zote kwa kuzingatia haki na usawa ili kukuza uchumi wa jamii na Taifa kwa ujumla.
Alisema
kauli mbiu hiyo inakinzana na hali halisi iliyopo katika jamii kutokana na
kuwepo kwa mfumo dume kwa baadhi ya makabila hali inayopelekea wanawake
kuonekana kuwa ni viumbe dhaifu ambao hawawezi kuwa na maamuzi yoyote katika
familia na jamii kwa ujumla.
Alisema Mila
na desturi kandamizi nayo ni sababu moja wapoinayo mfanya mwanamke kutopewa
fursa sawa na mwanaume hususani katika suala zima la Elimu kwani familia na
jamii kwa ujumla humpa kipaumbele mtoto wa kiume kuliko wa kike.
Mitula alitaja mambo mengine kuwa ni kukosekana kwa fursa ya kumiliki mali, na usawa katika suala zima la mirathi.
Katika
kuadhimisha maadhimisho hayo kwa kushirikiana na Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Jane Ng’ondi, Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya
Iramba walitembelea Hospitali ya Wilaya ya Kiomboi na kufanya matendo ya huruma
kwa kutoa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika wodi ya wajawazito na wazaza kama sabuni, maji, mafuta na
vingine vingi.
Akizungumza na wagonjwa hao wakati wa kukabidhi msaada huo Mwalimu Verian Masanja kutoka Kitengo KE Chama cha Walimu wilayani humo alisema wanaungana na wanawake wote hapa nchini na duniania kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu hiyo na kuwa wanaziunga jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuwaletea wananchi maendeleo.
Post A Comment: