Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wote nchini kuhakikisha wanashughulikia changamoto za Halmashauri ingali mapema kuliko kusubiria mpaka Tume ziunde kuja kuchunguza.


Bashungwa ameyasema hayo wakati akifunga Kikao kazi za Wakuu wa Mikoa cha kuwapitisha kwenye Sura ya Mipango na Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2022/23.


Amesema ninyi ni wasimamizi wa Halmashauri kwenye Mikoa yenu ikiwa mambo hayaendi sawa katika eneo lolote ni rahisi kujua mapema sasa kwanini msidhibiti changamoto hizo mnasubiria mpaka TAMISEMI tulete Tume wakati uwezo na Mamlaka mnayo? Alihoji Mhe. Bashungwa


Sasa nataka kuona mnachukua hatia

mapema kabla mambo hayajaharibika huko hii itasaidia kupunguza malalamiko na shughuli za maendeleo kutekelezwa kwa ubora. 


Halkadhalika Mhe. Bashungwa ameelekeza viongozi hao kusimamia ipasavyo Mfumo wa Nidhamu ya Watumishi katika Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa  ili kushughulikia watumishi wote wanaokwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.  


 Mhe. Bashungwa alihitimisha kikao hicho kwa kuwataka viongozi hao kuendelea  lkuongeza usimamizi kwenye Ukusanyaji wa

Mapato ya ndani ya Halmashauri ili kufikia Malengo ya kukusanya zaidi ya shilingi Trilioni moja kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.








Share To:

Post A Comment: