Mnamo tarehe 05-03- 2022 asubuhi katika eneo la mto mara Daraja la Mto Kirumi, asubuhi ilionekana uchafu wa maji yanayotembea kupitia mto huo kuelekea ziwani huku SAMAKI WAKIWA WAMEKUFA WENGI NA KUELEA JUU, na wakati huo maji yote ya eneo hilo hasa kijiji cha Kuruya yakiwa yamebadilika kabisa Rangi kutoka blue bahari na kuwa MEUSI KABISA huku juu ya maji hayo yakiwa yametanda mafuta, na maji yote yakiwa machafu sana.
Kifupi ilisemekana maji hayO yana viashiaria vya sumu na ndIo maana Samaki walikuwa wamekufa kwa wingi sana. Mbaya zaidi maji hayo ndiyo wakazi wa vijiji karibia vitatu vya maeneo yale wanatumia kwa matumizi ya nyumbani na hata kunywa.
Leo siku ya 5 hakuna hatua yoyote imechukuliwa huku maji hayo machafu yakiwa tayari yametapakaa sehemu ya eneo la ziwa huku watu wengine wanatumia maji hayo kwa matumizi ya nyumbani, mbaya zaid ndipo mradi mkubwa wa maji wa KYAMWAME na KINESI unao hudumia Vijiji zaidi ya saba kwa mradi wa Kyamwame na vijiji vitatu kwa mradi wa Kinesi, zaidi ya watu 15,000 kwa pamoja wanatumia maji ya ziwa kwa miradi hii peke yake.
Ni kweli MAELEKEZO yametolewa na nimshukuru sana DC wa wilaya ya Rorya kwa hatua za mwanzo alizochukua kwa kuzuia watu wasitumie maji ingawa tayari watu walikuwa washatumia zaidi ya siku tatu na hawana njia nyingine ya kutumia maji tofauti na eneo hilo kwa kuwa hakuna mbadala wake.
Niombe sana Serikali kupitia Waziri wa Mazingira, Waziri wa maji na waziri wa Afya walichukulie hili swala kwa uzito wake, kwa kuwa mpaka sasa hatujui watu/ wananchi wetu wamedhurika kwa kiwango gani, au hakuna madhara . Katika hili tujue-:
1. Nini athari kwa maisha yetu sisi binadamu kwa sumu ya maji haya.
2. Wapi na nani kasababisha haya maji yenye sumu kutiririka na kusababisha madhara makubwa kwa viumbe hai wa eneo hili ikiwa ni pamoja na Madhara tusiyoyaona kwa sasa kwa binadamu lakini huenda yakatokea badae.
3. Alifanya haya kwa malengo gani?
4. Kwa nini huyo mtu au Mgodi uliosababisha hawajafika eneo husika mpaka sasa kutoa elimu au hata kushirikiana na wananchi walioathirika na uchafu wa maji hayo yenye sumu.
5. Kama Kweli maji haya yana vimelea vya sumu nini haki sasa kwa wananchi hawa kisheria ili huyu mtu/ Mgodi husika kulipa fidia na kwa wananchi walioathirika.
Tunaomba kupata majibu ili kutoa na kuondoa sintofahamu inayoendelea kuzagaa ndani ya Wilaya ya Rorya.
Tukumbuke Rorya 77.6% imezungukwa na ziwa, maana yake kama kweli kuna vimelea vya sumu na imetapakaa kote ndani ya eneo hilo ama kando ya ziwa basi madhara ni makubwa kuliko tunavyo fikiri.
Niombe sana Serikali ichukue hatua za haraka kwa watu/ Mgodi huu ili kunusuru sio tu Maisha ya watu bali hata viumbe hai na vimelea vyote vya samaki vinavyoKufa bila huruma.
Asante
Chege
Mbunge Rorya
Post A Comment: