**************
Na. John Mapepele
Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Saidi Yakubu ameitaka Menejimenti ya Baraza la Kiswahili la Taifa ( BAKITA) kuwa wabunifu na kujiendesha kibiashara ili kuliingizia taifa mapato.
Yakubu amesema hayo leo Februari 6, 2022 alipofanya kikao na Menejimenti ya BAKITA na kukagua shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hiyo.
Amesema kwa sasa BAKITA linatakiwa kutumia fursa ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya kazi katika mikutano ya Umoja wa Afrika kupanua utendaji wa kazi zake nje ya Tanzania.
Aidha, Yakubu ameeleza kuwa BAKITA linaweza kuweka mikakati mbalimbali ya kubidhaisha lugha ya Kiswahili kwa kuingia ubia na wataalam na taasisi mbalimbali.
"Tuangalie fursa ya Kiswahili kwa kuuza zao hili kama pamba, au korosho ndani na nje ya nchi". Amesisitiza Yakubu.
Pia, amelitaka Baraza liendelee kujitangaza na kutangaza shughuli ambazo linazofanya ikiwa ni pamoja na ufundishaji na kuratibu ukalimani, ufanyaji wa tafsiri wa nyaraka mbalimbali na ufundishaji wa lugha.
Post A Comment: