Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.David Ndibalema akifungua Mkutano kati ya TBS na Wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi uliofanyika leo tarehe 17/02/2022 katika ukumbi wa mkutano Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora Bi.Ashura Katunzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano kati ya TBS na Wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi uliofanyika leo tarehe 17/02/2022 katika ukumbi wa mkutano Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi wakifuatilia mkutano kati yao na TBS uliofanyika leo tarehe 17/02/2022 katika ukumbi wa mkutano Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.David Ndibalema akipata picha ya pamoja na baadhi ya wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi wakati wa ufunguzi wa Mkutano kati ya TBS na Wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi uliofanyika leo tarehe 17/02/2022 katika ukumbi wa mkutano Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.David Ndibalema akipata picha ya pamoja na wakufunzi wakati wa ufunguzi wa Mkutano kati ya TBS na Wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi uliofanyika leo tarehe 17/02/2022 katika ukumbi wa mkutano Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.


*************************


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


Wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi wametakiwa kuhakikisha bidhaa zao zimekaguliwa na kukidhi viwango na Shirika la Viwango Tanzania ili kuondoa usumbufu na changamoto watakazozipata kule wanapopeleka bidhaa hizo.


Ameyasema hayo leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.David Ndibalema wakati akifungua Mkutano kati ya TBS na Wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi katika ukumbi wa mkutano Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.


Amesema cheti cha ubora wa bidhaa kinachotolewa na TBS kinafahamika kwa nchi nyingi hivyo ni bora kwa wafanyabiashara wakahakikisha bidhaa zao zimekaguliwa na kukidhii viwango pamoja na kupata cheti cha ubora ili kusiwe na changamoto za kukwama katika nchi za wenzetu.


"Kuna watu wanaweza wakakwama wakiwa wanapeleka kule bidhaa zao wakaombwa cheti cha ubora wa bidhaa zao wakashindwa kusaidika kutokana kuwa bado hawajafahamu majukumu ya TBS ". Amesema


Aidha Bw.Ndibalema amesema kupitia semina hiyo itatoa elimu juu ya majukumu ya TBS kulingana na huduma zinazotolewa na Wizara na Taasisi nyingine kwa wasafirishaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na chakula kwenda nje ya nchi pamoja na kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo hususani kwenye utaratibu wa usafirishaji wa bidhaa.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: