Mwandishi wetu ,Arusha


Umoja wa Vijama wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm) mkoani Arusha umeelezwa kuridhishwa na miradi inayotekelezwa na chuo cha ufundi Arusha (ATC) kupitia fedha za UVIKO-19 na nyingine zinatoka serikalini.


Kauli hiyo imetolewa Leo na mwenyekiti wa Uvccm mkoani Arusha ,Omary Lumato wakati alipoongozana na wajumbe mbalimbali wa baraza la umoja huo kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na chuo hicho.


Baadhi ya miradi inayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa hosteli za wanafunzi sanjari na jengo la mafunzo ya vitendo linalogharimu jumla ya kiasi cha sh,4 bilioni.


Akizungumza Mara baada ya kukagua miradi hiyo mwenyekiti huyo alisema kwamba umoja wao kwa niaba ya ÇCM wameridhishwa na utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na chuo hicho .


Lumato alisema kwamba miradi hiyo imesaidia kutoa ajira zaidi ya 10,000 kwa vijana mbalimbali nchini hali ambayo imesaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana nchini.


Lumato,alisema kwamba utekelezaji wa miradi hiyo imo kwenye ilani ya CCM na wanaishukuru serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi hiyo.


"Tunaishukuru serikali kwa kutoa fedha kugharamia hii miradi lakini pia tunafurahi kuona miradi hii imetoa ajira za kutosha hapa nchini" alisema Lumato


Naye mkuu wa chuo hicho,Dkt  Musa Chacha alisema kwamba wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha za kutosha kutekeleza miradi mbalimbali na wanahaidi kusimamia hizo kikamilifu.


Dkt ,Chacha alisema kwamba chuo chao kinawaandaa vijana wanaohitimu ili wakalete mchango na tija kwa taifa. 


Dkt  Chacha alisema kwamba kwa sasa chuo chao kinajipanga kuitumia miradi hiyo ili iweze kuzalisha fedha ambayo itawasaidia  kulipa mishahara pamoja na mahitaji mbalimbali.  


Baadhi ya miradi inayotekekezwa katika chuo hicho ni ujenzi  bweni la  Wasichana ambapo serikali imetoa  jumla ya Sh,bilioni  1.4 kama ruzuku kutoka serikalini  lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 428 Mradi ulianza mwishoni mwa mwezi Mei, 2021. 


Mradi mwingine ni  Ujenzi wa Jengo la Madarasa mbalimbali na Maabara  ya kisasa unaogharimu kiasi cha zaidi ya  3  billion.


Mwisho.

Share To:

Post A Comment: