Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na ugeni kutoka nchi ya Qatar (hawapo pichani) ambapo kikao hicho kilifanyika katika kumbi wa Mkutano uliopo hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Februari 18, 2022. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na ugeni kutoka nchi ya Qatar (hawapo pichani) ambapo kikao hicho kilifanyika katika kumbi wa Mkutano uliopo hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Februari 18, 2022.Kikao kikiendelea Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Mhe.Mohamed hassan Al Obaidali akizungumza mara baada ya kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Mhe.Mohamed hassan Al Obaidali mara baada ya kufanya mazungumzo katika ukumbi wa Mkutano uliopo hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Februari 18, 2022. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Mhe.Mohamed hassan Al Obaidali mara baada ya kufanya mazungumzo katika ukumbi wa Mkutano uliopo hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Februari 18, 2022. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar Mhe.Mohamed hassan Al Obaidali mara baada ya kufanya mazungumzo katika ukumbi wa Mkutano uliopo hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Februari 18, 2022.
*************************
Na: Mwandishi Wetu – Dar es Salaam
Tanzania imekusudia kuendeleza uhusiano uliopo kati yake na nchi ya Qatar, sambamba na kukuza mahusiano ya kibiashara, uchumi na fursa za ajira.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipokuwa na mazungumzo na ugeni kutoka nchi ya Qatar ambapo kikao hicho kilifanyika katika kumbi wa Mkutano uliopo hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Februari 18, 2022.
Waziri Ndalichako ameeleza kuwa, Tanzania na Nchi ya Qatar zimekuwa na mahusiano mazuri kwa muda mrefu na mataifa hayo yamekuwa yakishirikiana katika mambo mengi ikiwemo Biashara, Uwekezaji na shughuli nyingine nyingi zenye manufaa kwa nchi hizo mbili.
“Nipongeze Nchi ya Qatar kwa kuonyesha dhamira ya dhati katika utekelezaji wa makubaliano tuliyoingia tangu mwaka 2014 ambao umelenga kuimarisha uhusiano wa nchi zetu katika Nyanja mbalimbali zenye maslahi ya pande zote mbili,” alisema Profesa Ndalichako
Aliongeza kuwa, Tangu Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aingie madarakani amekuwa akionyesha dhamira yake ya dhati katika kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine na pia amekuwa akifungua fursa za uwekezaji nchini, ufanyaji wa biashara sambamba na kuwezesha watanzania kushirikiana na nchi rafiki katika nyanja mbalimbali.
Wakati huo huo, Waziri Ndalichako alipongeza nchi ya Qatar kwa kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia, hivyo alitumia fursa hiyo kuhamasisha ushirikishwaji wa vijana wa kitanzania katika fursa mbalimbali za ajira zitakazotolewa kuelekea katika maandalizi ya michuano hiyo.
“Tunafahamu mwaka huu 2022 Nchi ya Qatar itakuwa mwenyeji wa michuano wa Kombe la Dunia, hivyo mtambue kuwa nchi yetu imeendelea kuwaandaa vizuri sana vijana wake ili waweze kuwa na ujuzi ambao unahitajika katika nyanja mbalimbali ambao utawawezesha waweze kuajirika,” alisema
Naye, Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Kazi Qatar, Katibu Mkuu Mhe.Mohamed hassan Al Obaidali ameeleza kuwa kuridhishwa na mazingira yaliyopo nchini na Ukarimu wa Watanzania na kuahidi Serikali ya nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuangalia uwezekano wa kuwekeza kwenye miradi ya kiuchumi itakayoziletea maendeleo nchi hizo.
Post A Comment: