MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira akizungumza Bungeni Jijini Dodoma leo February 11,2022MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira akisisitiza jambo Bungeni Jijini Dodoma leo February 11,2022
NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
MBUNGE
wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh
Neema Lugangira ameiomba Serikali ipitie upya uamuzi wake wa kuondoa
masuala ya usalama wa chakula kutoka Wizara ya Afya na kuipelekea kwenye
eneo la mambo ya viwanda na biashara warudi kwenye best practice.
Aliyasema
hayo Bungeni leo Ijumaa tarehe 11 Februari 2022 Jijini Dodoma ambapo
alisema kwa sababu duniani kote masuala ya usalama wa chakula
yanaratibiwa na chini ya wizara ya afya kwa maana chini ya mamlaka ya
kudhibiti ubora wa chakula na dawa na hata kwa Tanzania miaka ya nyuma
tulikuwa tunafanya hivyo chini ya TFDA.
Mbunge
Neema alisema hata nchi za Afrika Mashariki zilikuja nchini kuja
kujifunza lakini miaka ya karibuni serikali ilivunja mamlaka hiyo na
badala yake kuunda TMDA na jukumu la usalama wa chakula wakaliweka chini
ya Shirika la viwango (TBS) sasa jambo hilo limeweka maisha na afya za
watanzania herani.
Alisema
anasema hivyo kwa sababu TBS ina jukumu la kuangalia ubora wa
matairi,misumari,mabati na nk na hapo hapo ipewe jukumu la kuratibu na
kudhibiti ubora na usalama wa chakula na hao hao ndio wanatoa kibali kwa
wazalishaji wa chakula .
“Na
hao hao waende kuangalia kile kibali kimekidhi kutakuwa na mgongano wa
maslahi, Mh Naibu Spika kuna jambo mahususi lilijitokeza ambalo ni
dhihiri kwamba TBS haiwezi kuendelea kubeba jukumu la usalama wa chakula
“Alisema
“Kwa mfano
mwaka jana Octoba 2021 Shirika la chakula na madawa la Kenya lilitangaza
kwamba linarudisha juice aina ya Seresi za Apple ambazo zilikuwa na
aina moja ya sumu kuvu ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu mpaka
siku hiyo kwa Tanzania TBS bado ilikuwa haijasema chochote”Alisema
Mbunge
huyo alisema na gazeti la Mwananchi lilimtafuta Mkurugenzi wa TBS na
anakumbuka alisema mpaka muda wa Octoba 14 mwaka 2021wamejiridhisha
juice hizo zilikiwa hazijaingia nchini na wanaendelea kufuatilia na
wakibaini zimeingia nchini zitazuiliwa .
Alisema
hapo wakauambia umma kila kitu kipo sawa kwa masikitiko makubwa TBS
waliwadanganya watanzania kwa sababu tarehe 22 kwenye kioski kimoja
Jijini Dodoma alikuta juice hizo aina ya Ceres ya Apple yenye Barcode
zile zile zinauzwa na alichukua jukumu la kuipiga picha na kumtumia
waziri mwenye dhamana ya viwanga na biashara na uwekezaji.
Aliongeza
kwamba baada ya Waziri huyo kupokea alisema ataifanyia kazi hilo
linaonyesha TBS hawakuchukulia kwa umakini jambo la usalama wa chakula
na hawana muda wa kuangalia usalama wa chakula na wanahatarisha maisha
ya watanzania kwa kuendela kulimbikiza mambo mengi ambayo mengine
hayaendani na usalama wa chakula
Mwisho.
Post A Comment: