Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilim akizungumza na wakazi wa Kata ya Kingolwira kufuatia tukio la mauaji ya Faidhat Ibrahimu (13) mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Msingi Mwenge lililotokea February 15, 2022.



 Na Farida Said, Morogoro

Siku chache baada ya faidhat ibrahimu (13) mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo katika Kata ya Kingolwira Manispaa ya Morogoro kuuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na kaka yake, Jeshi la polisi mkoani Morogogo limebaini kuwa muuaji huyo alitumia panga la mama yake kutekeleza mauaji hayo huku akiwa ameshawahi kumuua Bibi yake kutokana na imani za kishirikiana ambazo zimemfanya kushindwa kufanya tendo la ndoa tangu kuzaliwa kwake.

Kufuatia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Morogoro SACP Fortunatus Musilim amefika katika kata ya Kingolwira na kuzungumza na wananchi wa kata hiyo huku akiwataka kutoa taarifa za matukio ya uvunjifu wa amani katika maeneo hayo.

“Ukiona kuna mtu humuelewi elewi katika eneo lako toa taarifa hata kwa mwenyekiti wa mtaa yeye atatuletea taarifa sisi na tutazifanyia kazi hizo taarifa, msiwafiche wahalifu katika maeneo yenu.” Alisema Kamanda muslim.

 Kamanda Muslimu amesema matukio mengi ya mauaji yanatokana na migogoro ya familia, mmomonyoko wa maadili pamoja na imani za kishirikina jambo linalosababisha kujengeana chuki na kusababisha uvunjifu wa amaini katika jamii.

Aidha kamanda Musilim amewataka wananchi mkoani hapa kuhakikisha wanashirikiana na jeshi la polisi katika  kutoa taarifa za migogoro kwenye familia ili kudhibiti vitendo vya mauaji.

Kwa upande wao wananchi wa Mtaa wa Tambuka reli wameliomba JESHI la polisi kutoa ushirikiano kwa muda muafaka pindi matukio ya uharifu yanapoeipotiwa na wananchi hali itasaidia kukomesha matukio ya uharifu.

Share To:

Post A Comment: