Watu wengi huingia katika mkumbo wa kunywa pombe kwa namna ambayo ni hatari kwa afya zao.
Madhara ya muda mrefu yaweza kuwa kudhoofika mwili kwa kupoteza virutubisho, na kupoteza hamu ya kula, magonjwa ya ini kama kansa ya ini (hepatoma), magonjwa ya figo na ya moyo, kisukari, magonjwa ya akili nk. Hata hivyo kuna mbinu kadhaa za kuepuka madhara hayo kwa kiasi cha kuridhisha. Mbinu hizo ni kama ifuatavyo,
1. Fahamu aina ya pombe inayokufaa, usichanganye pombe kama sio mtaalam wa vinywaji.
2. Tambua wakati muafaka wa kunywa pombe, jifunze kujizuia ili utimize majukumu mengine na kujijengea heshima.
3. Kiasi, kuwa na kiasi chako maalum, usibugie. Kunywa kwa kiasi unachomudu kwa muda uliojipangia. Kwa hiyo ikiwa una muda mwingi unaweza kunywa taratibu ili isiishe haraka.
4. Mahali, si kila mahali ni salama kwa kunywa pombe, chagua mazingira yenye usalama, au karibu na nyumbani ama uwe na marafiki wawili au zaidi na wastaarabu kama wewe,
5. Kuwa mwangalifu na vinywaji vipya ambavyo hukuwahi kunywa.
6. Ikiwa unatumia dawa fulani, ni vema kuwasiliana na daktari wako akushauri endapo hazina madhara zinapokutana na pombe mwilini.
7. Jenga tabia ya kula vyakula vyenye wanga, mfano ugali kabla ya kunywa pombe au maji na juisi au vyakula vyenye mafuta, mfano nyama wakati ukiendelea kunywa pombe.
8. Heshimu haki za wasio kunywa pombe, si vizuri unapokuwa umekunywa pombe kuanza kugombana na mtu asiyekunywa. Wengine wana imani tofauti wanaweza kukujeruhi halafu usikumbuke chochote baadae pombe itakapoisha.
9. Usijiruhusu kulewa sana unapokunywa na watu usiofahamiana nao, au katika mazingira mageni.
10. Jizuie kunywa unapokuwa na hisia hasi, mfano Hasira, msongo wa mawazo, mfadhaiko nk. Pombe haipunguzi mawazo, inaweza kupelekea ufanye jambo baya zaidi. Kunywa pombe unapokuwa na furaha. Asante
Post A Comment: