Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara Mhe. Kanali Michael Mntenjele akizungumza na timu ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walipofika wilayani humo kwa ajili ya kufanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango inayoendelea mkoani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara Mhe. Kanali Michael Mntenjele akizungumza na timu ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walipofika wilayani humo kwa ajili ya kufanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango inayoendelea mkoani humo.

Afisa Msimamizi Mwandamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Fredy Mwesiga akimsikiliza kwa makini mfanyabiashara wa mapambo ya magari wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara Bw. Soti Warioba wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea wilayani humo.

Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Stephen Kauzeni akitoa elimu ya kodi kwa waendesha Pikipiki maarufu kama Bodaboda wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea wilayani humo.

Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Stephen Kauzeni akikagua risiti za EFD na kutoa elimu ya umuhimu wa kudai risiti kwa mfanyabiashara wa rejereja ambaye amenunua bidhaa kutoka kwa mfanyabiashara wa jumla wilayani Tarime katika Mkoa wa Mara wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea wilayani humo. (PICHA ZOTE NA TRA).

********************
Na mwandishi wetu
Tarime

Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara Mhe. Kanali Michael Mntenjele amewataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango inayofanyika wilayani humo ili waweze kutoa changamoto zao na kupata ufumbuzi.

Akizungumza na timu ya maofisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanaofanya kampeni hiyo ya elimu kwa mlipakodi wakati walipowasili wilayani humo, Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa, ni muhimu wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya kodi ili waweze kuelewa faida za kodi wanazolipa ndani ya nchi yao.

“Nitoe wito kwa wafanyabiashara wetu wa Tarime kama walipakodi wajitokeze kwa wingi na wawapokee waelimishaji wa TRA ili waweze kuwasilikiliza kwa lengo la kupata elimu ya umuhimu wa kulipa kodi kwasababu kodi hizo ndizo zinazoisaidia serikali kupata fedha kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa jamii”, alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Tarime.

Kwa upande wake mfanyabiashara wa nguo wa wilayani humo Bi. Zuhura Ally amesema kwamba, amefurahishwa na zoezi hilo ambapo amepata fursa ya kutoa changamoto zake ambazo zimefanyiwa kazi na maofisa hao wa TRA.

“Kwakweli ni jambo zuri TRA kujua wafanyabiashara tunaendeleaje na leo wameweza kutatua baadhi ya changamoto zangu na nyingine wameniambia nifike ofisini ili niweze kutatuliwa zaidi matatizo yangu,” alieleza Bi. Zuhura.

Nae mfanyabiashara wa mapambo ya magari wa wilayani humo Bw. Soti Warioba ameeleza kuwa, maofisa wa TRA wamebadilika sana tofauti na kipindi cha nyuma kiasi kwamba walipokuwa wanazunguka kwenye maduka mbalimbali kutoa elimu, hakuna mfanyabiashara aliyeogopa wala kufunga maduka.

Timu ya maofisa wanaofanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango mkoani Mara wako wilayani Tarime wakiendelea kutoa elimu ya kodi na baada ya wilaya hiyo wataelekea wilaya nyingine zilizopo ndani ya mkoa huo.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: