Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija , akizungumza na Wafanyabiashara Sokoni hapo



Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma akikazia jambo mbele ya mkuu wa Wilaya ya Ilala mara baada ya kutembelea soko la Zingiziwa.


Na Humphrey Shao

MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija ametoa agizo Kwa jeshi la Polisi kuwaondoa wafanyabiashara wote waliovamia eneo la Barabarani Chanika kuanzia leo

Mkuu wa Wilaya Ludigija ametoa agizo hilo katika ziara yake ya kutatua KERO soko la Zingiziwa Wilayani Ilala.

"Ninaagiza kuanzia Leo wafanyabiashara wote wanaofanya biashara Usiku Barabara ya Chanika kuondoka mara moja kwenda kufanya biashara katika maeneo yaliopangwa na Serikali ."alisema Ludigij

Ludigija alisema kwa Sasa Serikali imetoa shilingi milioni 100 Kwa ajili ya kuboresha soko la Zingiziwa hivyo imewataka wafanyabiashara kwenda katika soko hilo sio kufanya biashara Barabara.

Amesema Serikali haipendi kutumia nguvu hivyo amewataka wafanyabiashara wote kwenda kufanya biashara zao katika masoko.

Amesema marufuku kufanya biashara Chanika Barabarani,watakaofanya biashara wataondolewa na Serikali .

Aliagiza Chama Cha Mapinduzi na Ofisi ya Diwani Zingiziwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala katika kutatua changamoto za soko hilo.

Aidha alisema eneo hilo la Serikali Mali ya soko hivyo aliwataka wafanyabiashara wote kupata maeneo ya Biashara sokoni hapo.

Akizungumzia Barabara ya Zingiziwa Sokoni alisema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inaanza kukarabati sambamba na kuweka vifusi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Zingiziwa Maige Maganga alisema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ina masoko zaidi ya 200 ikiwemo soko Hilo la Zingiziwa.

Amewataka wafanyabiashara wa soko la Zingiziwa kuacha kuja na Ramani zao mifukoni kujenga vibanda sokoni hapo, badala yake wafanyabiashara wote wametakiwa kuvunja vibanda walivyojenga na kufuata taratibu Ofisi ya Afisa Mtendaji Zingiziwa Kwa ajili ya kupatiwa eneo la Biashara.

Ameiagiza Serikali kuomba Daladala zote za Chanika ,Mvuti na Zingiziwa kuingia sokoni hapo kushusha abiria Kwa ajili ya kutangaza soko hilo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma alisema dhumuni la ziara hiyo kwasabu simu zilikuwa nyingi za wafanyabiashara Ofisi za chama Kwa ajili kuja kutatua changamoto .

Ubaya Chuma alisema chama Cha Mapinduzi ndio watekelezaji wa Ilani inaishauri Serikali katika kushirikiana na kutatua changamoto mbali mbali.

Share To:

Post A Comment: