Jane Edward,Arusha


Waziri  wa kilimo,Profesa  Adolph Mkenda amezitaka halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu ili wakulima kupata mbegu bora ambazo za aina mbalimbali za mazao ambazo zitazalishwa kwa wingi na kuwafikia kwa  urahisi wakulima ili waweze kulima na kukifanya kilimo kiwe chenye tija


Waziri Mkenda ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa uzalishaji wa mbegu jijini Arusha ambapo amezitaka halmshauri za wilaya ambazo zinatoza ushuru wa kusafirisha mbegu za mazao kuacha mara moja kwani hakuna sheria inayo ruhusu kutoza ushuru wa mbegu.


Amesema kuwa kuanzia sasa serikali itayadhibiti makampuni ambayo yanazalisha mbegu za mazao mbalimbali zisizo na ubora lengo ni kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora na mbegu zote zitakuwa na Lebo maalumu kuonyesha ubora wake


Aidha Waziri Mkenda, amesema kuwa serikali itendelea kusimamia upatikanaji wa mbegu  bora za mazao  mbalimbali ili uwezesha kuwepo kilimo chenye tija ambacho kinatoa mazao mengi na kusisitiza kwamba mageuzi ya kilimo  lazima yaanze na uzalishaji wa mbegu  bora


Amesema kuwa  serikali itaongeza fedha za utafiti na uzalishaji wa mbegu bora sanjari na kusomesha vijana  kwenye vyuo mbalimbali mahiri duniani katika ngazi za masta na PHD kwa kuwa wataalamu waliopo wanastaafu.


Waziri,Mkenda,ameziomba  benki nchini kuwekeza kwenye sekta ya kilimo  kutokana na kutambua kuwa changamoto inayoikabili sekta ya kilimo ni  upungufu wa fedha hivyo benki zinayo nafasi kubwa ya kusaidia kuboresha kilimo nchini kwa kuwa kilimo kina faida.


Waziri Mkenda, amesema kuwa wizara imeomba ipewe yaliyokuwa mashamba ya kilimo cha maua yaliyopo mkoani Arusha, ambayo wamiliki wake wameacha kuyaendeleza ili yaweze kutumika kuzalisha mbegu bora na kufanya utafiti.


 


Baldwin  Shuma Mkurugenzi mtendaji TASTA anasema maeneo ya kuzalishia mbegu ni muhimu ili kutunza mbegu zinazopatikana hapa nchini na hiyo itazuia uagizwaji wa mbegu  nje ya nchi


Ameongeza kuwa ni wakati sasa kama nchi kuongeza wawekezaji kutoka nje ili kuwekeza kwenye sekta ya mbegu ambapo sekta binafsi inaangalia ina mbegu za kutosha lakini pia wakulima kujitathimini kama wana mbegu na wao kama tasta wamejipanga wamejipanga vizuri


Kwa upande wake  mkurugenzi wa biashara kampuni ya Quincewood group ltd ,Fatma Fernandes, amesema  wameanzisha mfumo  wa mawakala wa sekta ya kilimo nchini unaowawezesha kununua na kuuza mbegu bora na kuweka kumbukumbu  za mauzo na mikopo waliyoitoa na wao wataichakata na kuiwasilisha serikalini.


Amesema mfumo huo umebuniwa kwa kushirikiana na Agra,na tayari wapo katika mikoa saba ambapo tayari mawakala 600 wameshajiunga na mfumo huo ambao unarahisisha  mbegu kumfikia mkulima hivyo mfumo huo ni mkombozi ,lengo lao ni kuhakikisha mfumo huo unaenea nchi nzima.

MWISHO…………..

Share To:

Post A Comment: