Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto za kiutumishi zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwabakizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto za kiutumishi zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Bw. John Kayombo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri yake kwa Katibu Mkuu, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto za kiutumishi zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo.
Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Bw. Didas Asenga akiwasilisha hoja kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto za kiutumishi zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akisikiliza hoja za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto za kiutumishi zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo.
Afisa Utumishi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Ernest Ngate akisikiliza hoja ya mmoja wa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji wakati wa ziara Katibu Mkuu-UTUMISHI iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto za kiutumishi zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo.
Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Bw. Costantine Mnemele akitoa neno la shukurani kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto za kiutumishi zinazowakabili katika Halmashauri hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa pili kulia) akisikiliza taarifa ya hali ya kiutumishi ya Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji iliyowasilishwa kwake na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Bw. John Kayombo (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabilili watumishi wa Halmashauri hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji mara baaada kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto za kiutumishi zinazowakabili watumishi wa katika Halmashauri hiyo.
*******************************
Na. Nasra H. Mondwe - Rufiji
Tarehe 17 Novemba, 2021
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewataka Watumishi wa Umma kusimamia vema matumizi ya shilingi trilioni 1.3 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ustawi wa taifa.
Dkt. Ndumbaro ametoa wito huo kwa Watumishi wa Umma, wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
Dkt. Ndumbaro amesema, hivi karibuni Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alipokea shilingi trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) na kuzielekeza katika ujenzi wa madarasa, vituo vya afya na ununuzi wa vifaa mbalimbali, hivyo ni jukumu la Watumishi wa Umma kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati uliopangwa.
“Miradi ya ujenzi wa madarasa na zahanati inatakiwa kukamilika ndani ya miezi tisa tangu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan azindue rasmi tarehe 10 Oktoba, 2021 jijini Dodoma, na sisi Watumishi wa Umma ndio tunao wajibu wa kusimamia,’’ Dkt. Ndumbaro amesisitiza.
Akizungumzia uadilifu katika utekelezaji wa miradi hiyo, Dkt. Ndumbaro amewaasa watumishi wenye dhamana ya manunuzi kutokwamisha miradi hiyo kwa masilahi binafsi na badala yake wawe ni sehemu ya kuwezesha miradi yote kukamilika katika muda uliopangwa.
“Wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo, Mhe. Rais alishauri utumike utaratibu wa manunuzi wa single source ili kupunguza urasimu katika ununuzi wa vifaa vya ujenzi, hivyo tunapaswa kuzingatia,” Dkt. Ndumbaro amesisitiza.
Aidha, Dkt. Ndumbaro amewakumbusha watumishi wote wa umma kuwa, hakuna haki bila wajibu na kuwataka kutimiza wajibu wao ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa upande wake imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Watumishi wa Umma wanapata stahiki zao kwa wakati.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Mhe. Juma Ligomba amemshukuru Dkt. Ndumbaro kwa kufanya ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma wa Halmashauri hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro amehitimisha ziara yake ya kikazi wilayani Rufiji iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kuwasikiliza Watumishi wa Umma na kutatua kero na changamoto za kiutumishi zinazowakabili.
Post A Comment: